Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania

Habari

WANAWAKE TUME YA KUREKEBISHA SHERIA TANZANIA WATOA MSAADA KWA WAZEE WASIOONA KITUO CHA MATEMBE BORA DODOMA


Kuelekea siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Machi 8, kila Mwaka, Wawanawake wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania watoa Msaada wa Chakula na Mavazi katika kituo cha Wenye Mahitaji maalum cha Watu wazima wasioona Matembe Bora Buigiri mkoani Dodoma.

Akizungumza wakati wa kukabidhi misaada hiyo Machi 7, 2024 Naibu katibu Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bi. Zainab Chanzi, alisema pamoja na Tume hiyo kuwa na majukumu kadhaa ikiwamo kutoa elimu ya sheria kwa wananchi ili waweze kuzifahamu na kuzitekeleza ameeleza Taasisi hiyo pia kuona umuhimu wa kurudi kwa jamii ambapo kuelekea siku ya wanawake Duniani iliamua kujumuika na Wazee hao Wasioona na kuwapatia mahitaji mbali mbali ya kujikimu.

“Taasisi iliona ni vizuri kurudi kwenye jamii na tuliona ni vizuri kuja katika kituo hiki cha watu wenye mahitaji maalum tujumuike nanyi kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani , wanawake ni chachu ya maendeleo katika Jamii” Alisema Bi. Zainab

Akitoa shukrani zake kwa niaba ya wakazi wa Kituo hicho baada ya kupokea Msaada huo Yeled Cheleso ambae ni Mwenyekiti wa kituo cha Watu wazima wasioona Matembe bora ameishukuru Tume kwa Msaada huo na kuwaomba kuendeleza utaratibu huo ili kuwapunguzia changamoto zinazowakili za mahitaji mbali mbali ya kujikimu.

“Tunawashukuru sana Tume kwa Msaada huu, tunawaomba muendelee kutusaidia kila mnapopata nafasi msituchoke na karibuni sana” alisema Cheleso

Kituo cha Wenye Mahitaji Maalum cha Watu Wazima Wasioona Matembe Bora kilianzishwa Mwaka 1992, kwa sasa kituo kina kaya 13 ambapo pamoja na changamoto ya ulemavu waliyonayo lakini wamekua wakishughulisha na shghuli za Ujasiliamali, kilimo na Ufugaji.