Utafiti wa Sheria
Mkuu wa Kitengo - Juliana E. Munisi
Majukumu:
- Kufanya utafiti wa awali na kupendekeza maeneo yanayohitaji maboresho ya kisheria.
- Kuandaa andiko la awali, Taarifa ya majadiliano na taarifa yenye mapendekezo ya maboresho ya sheria.
- Kufanya utafiti kwa ajili ya maboresho ya sheria.
- Kuainisha na kuchambua taarifa za kisheria zilizoandaliwa na taasisi nyingine, wataalamu elekezi na taarifa za watafiti wa kisheria zenye mlengo wa maboresho ya kisheria.
- Kushauri Taasisi za Serikali katika masuala yanayohitaji maoni ya /msaada wa kisheria.
- Kutathmini mikataba mbalimbali iliyoridhiwa na Serikali, makubaliano, itifaki na nyaraka nyinginezo za kikanda na kupendekeza kwa Serikali namna ya kuziasili.
- Kuratibu program za mabadiliko ya kisheria yanayoendelea ambayo yanaendana na programu za shughuli za Tume.
- Kuendesha warsha na makongamani yanayohusiana na maboresho ya sheria.