Ununuzi na Ugavi
Majukumu ya Kitengo cha Ugavi na Ununuzi
Mkuu wa Kitengo - Nessy E. Kyejo
- Kusimamia ununuzi wowote na uuzaji wa mali za Wizara kwa njia ya Zabuni isipokuwa usuluhishi na kutunuku zabuni ;
- Kuratibu shughuli za Bodi ya Zabuni ya Wizara;
- Kutekeleza maamuzi ya Bodi ya Zabuni ya Wizara;
- Kufanya kazi kama Sekritarieti ya Bodi ya Zabuni ya Wizara
- Kuandaa mpango wa Ununuzi na Uuzaji wa mali za Wizara kwa njia ya Zabuni;
- Kupendekeza ununuzi na uondoshaji wa mali za Wizara kwa utaratibu wa zabuni;
- Kukagua na kuainisha upungufu wa mahitaji katika Wizara na kutoa tamko kuhusu mahitaji hayo;
- Kuandaa nyaraka za zabuni kwa ajili wazabuni kushiriki;
- Kuandaa matangozo ya fursa za zabuni;
- Kuandaa rasmu za Mikataba;
- Kutoa mikataba iliyothibitishwa na kusainiwa;
- Kuandaa na kuhifadhi kumbukumbu za mchakato wa ununuzi na uuzaji wa mali za Wizara;
- Kuandaa na kutunza orodha au kitabu cha mikataba yote ambayo Wizara imetunuku;
- Kuandaa taarifa za kila mwezi kwa ajili ya Bodi ya Zabuni ya Wizara;
- Kuandaa taarifa ya kila robo ya mwaka juu ya utekelezaji wa mpango wa ununuzi na kuwasilisha katika kikao cha menejimenti ya Wizara;
- Kuratibu kazi za ununuzi na uondoshaji wa mali za serikali katika Idara na vitengo vyote vya Wizara; na
- Kuandaa taarifa nyinginezo kadri zitakavyo hitajika muda wowote.