Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa pamoja na Wakuu wa Mashtaka wa Mikoa wakiwa wanatoa maoni kuhusu tahthmini na utafiti wa sheria zinazohusu makosa dhidi ya Maadili Jana kwenye ukumbi wa NBS jijini Dodoma.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Ndg. Griffin Mwakapeje akitoa ufafanuzi katika kikao cha kukusanya maoni na tathmini ya Sheria dhidi ya makosa ya maadili , kikao hicho kilihudhuriwa na Wakuu wa Wapelelezi wa mikoa pamoja na wakuu wa mashtaka wa mikoa (Hawapo pichani) kutoka Tanzania bara na Visiwani, tarehe 12 na 13 Mei 2023 jijini Dodoma .
Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Jaji Mstaafu January Msoffe(katikati) akiwa ameongoza kikao cha majadiliano ya kukusanya maoni ya tathmini na utafiti wa sheria mbalimbali zinazohusu makosa dhidi ya maadili tarehe 12 Mei 2023 Jijini Dodoma.
Wanasheria wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania wakiwa katika picha ya Pamoja na Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bw. Griffin Mwakapeje, Mara tu baada ya kuhitimishwa kwa Kongamano la Kitaifa la Sheria ya ndoa Tanzania, lililofanyika Ukumbi wa Morena Hotel tarehe 24/04/2023
Baadhi ya Watumishi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Dr. Damas Ndumbaro, katika Ukumbi wa Hotel ya Morena Dodoma
Watumishi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi Mary Makondo (Katikati waliokaa) mara baada ya uzinduzi wa kikao cha 18 cha Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania, kilichofanyika katika ukumbi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliyopo Njedengwa Dodoma
Menejimenti ya Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi Mary Kondo (Katikati waliokaa) mara baada ya uzinduzi wa kikao cha 18 cha Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania, kilichofanyika katika ukumbi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliyopo Njedengwa Dodoma
Muwezeshaji wa mada ya Afya ya Akili Dokta Roselyne Malenya kutokea Hospital ya Mirembe akitoa mada kwa wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania, katika kikao cha 18 cha baraza hilo kilichofanyika katika ukumbi wa Tume ya taifa ya Uchaguzi Njedengwa - Dodoma.
Bi Moshi J. Muna Mtumishi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Bahi Mh. Godwin Gondwe kipeperushi cha Elimu ya Sheria kwa umma kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania
Wanawake Watumishi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT) wakiwa katika maandamano ya Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Wanawake Duniani, maadhimisho hayo yalifanyika katika Viwanja vya Sabasaba Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma, yakiwa na Kaulimbiu "UBUNIFU NA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA CHACHU KATIKA KULETA USAWA WA KIJINSIA."
Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar (Kushoto) akimkabidhi kalenda za Matukio muhimu ya Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar Bw. Griffin Venance Mwakapeje (Kulia), Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania.
Katibu mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Ndugu Griffin Venance Mwakapeje, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Natu El-Maamry Mwamba na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Ndugu Emmanuel Mpawe Tutuba wakila Kiapo cha Maadili kwa Viongozi, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 09 Januari, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Moses Mpogole Kusiluka, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Ndugu Emmanuel Mpawe Tutuba, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria Ndugu Griffin Venance Mwakapeje na Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Sivangilwa Mwangesi mara baada ya hafla ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 09 Januari, 2023.