Fedha na Uhasibu
Mkuu wa Kitengo - Margareth Ndebelamatwi
Majukumu ya Kitengo cha Fedha na Uhasibu
- Kutekeleza jukumu la ulipaji fedha kwa kuzingatia taratibu na miongozo iliyopo na kuhakikisha watu wanafuata sheria na taratibu za fedha kwa makundi mbalimbali yakiwemo;
- Madai ya watumishi na stahili zao mfano malipo ya likizo, safari na madai mengineyo.
- Kulipa stahili za viongozi kisheria
- Kulipa mishahara
- Madai mbalimbali ya viongozi mfano fedha ya safari
- Kulipa watoa huduma mbalimbali zilizotokana na mikataba mfano, ulinzi, usafi, huduma za internet, simu, umeme na kadhalika
- Kulipa gharama ya matengenezo ya magari na vifaa mbalimbali vya ofisi
- Kulipia ,manunuzi mbalimbali mfano shajala na kadhalika
- Utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka za fedha
- Kuandaa taarifa za kila mwezi, kila robo ya mwaka, nusu mwaka na kuwasilisha Hazina
- Kuandaa taarifa za hesabu kwa mwaka mzima wa fedha “Annual Final Accounts”
- Kutoa majibu na kufuatilia majibu toka Idara mbalimbali na Vitengo kutokana na Hoja za Ukaguzi, hii inahusu hoja za mkaguzi wa ndani na nje
- Kuandaa majibu kutokana na “Management letter” anayoitoa Mkaguzi wa Nje, kutokana na utendaji wa mwaka mzima wa wa Wizara kwa Idara na Vitengo vyote.
- Ufuatiliaji wa masuala ya PAC endapo Wizara itatakiwa kuhudhuria mbele ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali.
- Utoaji taarifa kuhusu maduhuli yaliyokusanywa na Wizara
- Kusimamia vikao viwili kabla na baada ya Ukaguzi (Entry and Exit Conference)
- Usimamizi wa Special Funds kama zipo
- Kutoa ushauri kwa Afisa Masuhuli kuhusiana na Masuala ya fedha.