Tume
TUME
Tume ya Kurekebisha Sheria (“Tume”) inakukaribisha katika tovuti yake. Katika ukurasa huu utaielewa Tume na kupata yaliyomo ndani yake.
Chimbuko la historia ya Tume linatokana na Taarifa ya Tume ya Mapitio ya Mfumo wa Mahakama ya mwaka 1977 maarufu kama (“Tume ya Msekwa”). Taarifa hii ilisisitiza juu ya hitaji la kuhakikisha sheria za Tanzania zinaendana na wakati na mabadiliko ya jamii inayobadilika ya kitanzania.
Ni kutokana na Taarifa hii, Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania ilianzishwa mwaka 1983 chini ya Sheria ya Tume ya Kurekebisha Tanzania, Sura 171. Miongoni mwa mamlaka ambazo Sheria iliyoanzisha Tume imetoa ni pamoja na mamlaka ya Tume:
1.Kuboresha Sheria zote za Tanzania kwa lengo ya kuzifanya ziendane na hali ya sasa ya kijamii na kiuchumi;na
2.Kupendekeza kutungwa kwa sheria pale ambapo hakuna sheria.
Tangu kuanzishwa kwake Tume imeongozwa na wenyeviti wafuatao:
1.Mh. Jaji Yona Mwakasendo (1983- 1984);
2.Mh. Jaji Damian Lubuva (1984 - 1985);
3.Mh. Jaji Hamisi Msumi (1986 - 1990);
4.Mh. Jaji Raymond Mwaikasu (1991 - 1995);
5.Mh. Jaji Anthony Bahati (1995 - 2006);
6.Mh. Jaji Ibrahim H. Juma (2007 - 2013);
7.Mh. Jaji Aloysius Mujulizi(2013 - 2017);na
8.Mh. Jaji January H. Msoffe (2018 -2023).
9. Mh. Jaji Winfrida B. Korosso (2024)
Katibu wa Tume ndiye Mtendaji Mkuu wa Taasisi na msimamizi wa majukumu ya kila siku ya Taasisi. Katibu wa Tume na watumishi wengine wa Tume ndio wanatengeza uwepo wa Tume, Wafuatao ni watumishi mbalimbali wa Umma waliotumikia nafasi ya Katibu wa Tume:
- Bw.Nathaniel Issa- (1984- 1990);
- Mh. Jaji Mstaafu Stephen E.N. Ihema- (1990 - 1999);
- Mh. Jaji Mstaafu Bethuel M.K. Mmilla - (2000 - 2002);
- Mh. Jaji wa Mahakama Kuu,Mary S. Shangali - (2003 – 2003);
- Bw.Mathias M. Chikawe - (2003 – 2005).
- Bi. Crescencia W. Makuru –(2006 – 2008)
- Bw.Japhet Sagasii (2008 - 2011).
- Bi. Winfrida B. Korosso (2012 – 2014)
- Bw.Casmir Kyuki (2015-7/1/2023)
- Griffin Mwakapeje ( Jan.9,2023 - sept 13, 2023)
- George Nathaniel Mandepo (03 Oct. 2023 -)