Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania

Habari

SERIKALI INAENDELEA KUTAFSIRI SHERIA KWA LUGHA YA KISWAHILI - NAIBU KATIBU LRCT


Serikali inaendelea na mchakato wa kutafsiri Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ziweze kutumika kwa lugha ya kiswahilina kingereza ili kueleweka vizuri kwa watanzania walio wengi.

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 4/07/2024 na Naibu Katibu Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT) Bi Zainab Chanzi wakati akijibu maswali ya wananchi waliotembelea Banda la Tume hiyo walipotaka Kujua kwa nini Sheria nyingi zimeandikwa kwa lugha ya kingereza ambacho watanzania wengi hawakijuwi.

Naibu Katibu amesema kwamba Kazi hiyo inaendelea kufanywa na serikalichini ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG) kupitia kwa Mwandishi Mkuu wa Sheria ambapo miswada mbalimbali imekuwa ikiandaliwakwa nakala za lugha za kingereza na kiswahili.

"Serikali inaendelea na mchakato wa kutafsiri Sheria ziwe kwa lugha ya kiswahili na kingereza kazi inayofanywa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kazi hii inahitaji muda na utulivu wa Hali ya juu ili Sheria iweze kubaki na malengo ya awali" alisema Zainab.

Hata hivyo aliwasisitizia kuendeleza Banda la Tume hiyo ili wapate misingi ya Sheria kwa kuwa wanatoa elimu ya Sheria kwa Umma.

Awali akiuliza maswali kuhusu Sheria kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili bwana Richard Wales alieleza kwamba wapo watu wanaoingia hatianikwa kushindwa kuisoma Sheria na kuielewa kwa kuwa imeandikwa kwa lugha ya Kingereza.

Bwana Walesi alieleza Jambo hilo kuwa na hatari ya kutowatendea haki wananchi na ni kinyume na maandiko ya mwenyezi Mungu.