Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania

Utawala na Rasilimali Watu

Majukumu ya Kitengo cha Utawala na Rasilimali Watu

Kinaongozwa na Mohammed I. Mavura (Mkuu wa Kitengo cha Utawala na Rasilimali watu)

Madhumuni

Kitengo cha Utawala na Rasilimali Watu ni mhimili wa Uendeshaji wa shughuli za Taasisi hii za kila siku. Katika kutekeleza wajibu wake Idara inamsaidia Mtendajji Mkuu wa Wizara ambaye ni Katibu Mkuu kuiongoza Wizara. Aidha, Idara hii ina jukumu la kuhakikisha kuwa Taasisi ina nyenzo za kutosha za kufanyia kazi, nyenzo hizo ni pamoja na rasilimali watu, fedha, majengo, usafiri, samani, n.k. Idara ya Utawala na Rasilimali Watu pia inao wajibu wa kuwezesha Idara zingine “Line Departments” kutenda kazi zake. Pia ina jukumu la kusimamia utendaji kazi katika Taasisi kwa kuhakikisha kuwa malengo makuu ya Tasisi yanafikiwa.

Idara ya Utawala na Raasilimali watu imegawanyhika katika sehemu kuuu mbili:-

Sehemu ya Utawala/Uendeshaji:

(i)Kuhakikisha watumishi wanafuata Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma;

(ii)Kutafsiri Sheria na Kanuni za Utendaji kazi kwa watumishi katika eneo la kazi;

(iii)Kuhakikisha Tume ina vitendea kazi vya kutosha;

(iv)Kusimamia utendaji wa Masijala za Tume;

(v)Kushughulikia masuala ya Itifaki;

(vi)Kusimamia Usafiri, Ulinzi na Usalama wa Jengo;

(vii) Kusimamia matengenezo ya vitendea kazi vya Tume, Majengo na bustani;

(viii)Kusimamia ustawi wa wafanyakazi ikiwa ni pamoja na Afya, Usalama, Michezo na Utamaduni;

(ix)Kusimamia Maadili ya Utumishi wa Umma pamoja na kutoa elimu ya kuzuia na kupambana na Rushwa;

(x)Kusimamia masuala Mtambuka kama Jinsia, Ukimwi (HIV/AIDS) na kuwa mwakilishi wa masuala Mtambuka ;

(xi)Kuratibu masuala ya Sekta binafsi katika Tume;

(xii) Kuratibu Utekelezaji wa Mikakati ya Kuboresha Utendaji Tume;

(xiii)Kushauri juu ya mbinu za kuongeza Ufanisi Tume;

(xiv)Kuratibu Utekelezaji wa Mkataba wa Huduma kwa Mteja;