Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania

Habari

MWENYEKITI TUME YA KUREKEBISHA SHERIA TANZANIA AAGIZA KUUNDWA KAMATI NDOGO KUSHUGHULIKIA MIRADI YA TUME HIYO


Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Mhe, Jaji Winfrida B Korosso ameagiza kuundwa kwa kamati ndogo itakayoshughulikia utafutaji wa fedha za maendeleo ambazo zitasaidia katika utekelezaji wa majukumu ya Tume hiyo.

Agizo hilo amelitoa tarehe 24/05/2024 alipowasili Kwa mara ya kwanza katika ofisi hizo tangu alipoteuliwa na kuapishwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ambapo akiwa katika ofisi hizo alikutana na watumishi na kufanya Kikao kwenye ukumbi wa mikutano ambapo ameeleza umuhimu wa kufikia njia tofauti ya kutafuta fedha za maendeleo.

Mhe, Jaji Korosso amesema, utatuzi wa changamoto ya ukosefu wa fedha ni kuandaa watu wachache watakao shughulika na maandiko ya kuomba fedha kwa ajili ya maendeleo badala ya kutegemea Fedha za Oc pekee.

"Hapa Katibu wa Tume Bw. George Mandepo amenieleza kwamba moja ya changamoto ni upungufu wa fedha ambapo wanategemea OC pekee, nataka tuunde kamati ndogo watakaoshughulika na uandishi wa maandiko ya kuomba fedha za maendeleo na ufuatiliaji ukiwa ni pamoja na kubuni upatikanaji wa miradi mipya" alisema Korosso.

Aidha ameendelea kueleza kwamba ili Tume iweze kutatua changamoto ya fedha ni lazima kufikiria kwa njia tofauti katika kupata fedha za miradi.

Mhe. Jaji Korosso ameagiza Kitengo Cha elimu kwa Umma kuendeleza jitihada za kujitangaza hasa katika kipindi hiki ambacho Tume imeeanza kuaminika na kutambulika kiasi Cha kupewa kazi na Tume ya Haki jinai za kufanyia utafiti Sheria zinazosimamia maadili na adhabu mbadala.

Aidha amewataka Watumishi kuongeza juhudi katika kutekeleza majukumu yao huku akiwapongeza kwa kufanya kazi kubwa huku wakiwa na idadi ndogo ya Watumishi.

Awali Katibu Mtendaji Tume hiyo Bw,George Mandepo alisema pamoja na changamoto zinazowakabili lakini wameendelea kutekeleza tafiti mbalimbali ikiwemo mapitio ya Sheria ya biashara, Sheria inayosimamia vyama vya ushirikia, mapitio ya Sheria zinazosimamia dhamana,adhabu ya viboko na Sheria zinazosimamia ulinzi wa mashahidi.

George Mandepo amesema katika mwaka wa fedha 23/24 Tume ilikuwa na bajeti ya Tsh. Bilioni 5.1 ambapo ameeleza kwamba mpaka Sasa wamepokea zaidi ya aslimia 76 ya bajeti husika.