Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania

Elimu ya Sheria kwa Umma

Kitengo cha Elimu kwa Umma

Mkuu wa Kitengo - Zainab I. Chanzi

Majukumu:

1. Kuanzisha na kuimarisha mfumo wa ushirikiano, mashauriano na ushirikiano na vyombo vingine ndani au nje ya Tanzania vinavyojihusisha na maboresho sheria.

2. Kushirikiana na Taasisi za Serikali, asasi ya kijamii na mashirika yasiyo ya kiserikali katika michakato ya maboresho ya kisheria.

3. Kuanisha maandiko ya awali, taarifa ya Majadiliano na taarifa za taasisi nyingine na kisha kuishauri Serikali ipasavyo.

4. Kuendesha semina na warsha za usambazaji wa habari juu ya masuala yanayohusiana na maboresho ya sheria.

5. Kukusanya Mikataba, Itifaki, Sheria na kuziweka kwenye tovuti ya Tume.

6. Kubuni, kuandaa na kutoa Jarida la Sheria ya Tume kila mwaka.

7. Kubuni, kuandaa na kutoa vipeperushi na kalenda.

8. Kuratibu mikutano na waandishi wa habari kwa Tume.

9. Kubuni na kuandaa mipango ya uhamasishaji wa umma kupitia sheria kupitia vyombo vya habari.