Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania

Habari

Waomba Sheria ya Mtoto Kuangaliwa Upya


Wananchi wameiomba Serikali kupitia Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT) kuangaliwa upya Sheria ya Ulinzi na ustawi wa Mtoto ya mwaka 2009 kama inasaidia kuwalinda watoto kama ilivyotarajiwa kutokana na ongezeko la watoto wa mitaani hapa nchini.

Maombi hayo yametolewa na baadhi ya wananchi waliotembelea Banda la Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania wakati wa maonesho ya sabasaba yanayoendelea Mkoani Dar es Salaam wakati Tume hiyo ikiendelea Kutoa elimu ya Sheria ya kwa Umma.

Ramadhani Nyumbu kutoka Mkuranga mwenye miaka 56 amesema kwa Sasa watoto wa mitaani wamekithiri Kila eneo kwa Sababu ya wazazi kutotekeleza wajibu wao kwa watoto ikiwemo kuwapatia huduma muhimu ya chakula elimu na malezi bora Jambo ambalo ameeleza kwamba Sheria ya ulinzi na ustawi wa mtoto haijafanikiwa kudhibiti hilo.

"Inasikitisha Kuona watoto wapo mitaani wanazurura na Sheria ipo, kwanini hawakamatwi wakawaonesha wazazi walipo na Sheria ikachukua mkondo wake? aliuliza bwana Ramadhani.

Kwa upande wake Wakili wa serikali Ismaili Hatibu akijibu hoja hiyo alieleza kwamba Tume imelipokea na itaangalia endapo mapungufu yapo kwenye utoaji wa elimu ya Sheria au vinginevyo ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa