Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania

Habari

​TUME YA KUREKEBISHA SHERIA YATAKIWA KUITUPIA JICHO SHERIA ZA USAFIRI WA ARDHINI



Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania imetakiwakuangalia upya sheria za usafiri ardhini kwa kuzifanyia mapitio na utafiti wa kina kwa kuwa zimeonekana kutodhibiti kikamilifuajali za barabarani ili ziweze kuwalazimisha wamiliki wa vyombohivyo kuimarisha huduma na kuwapunguzia kazi madereva kwa kuendesha mwendo mrefu kama hatua za kupunguza ajali za barabarani.

Maelekezo hayo yametolewa leo tarehe 03/06/2024 na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Pindi Chana wakati akifungua kikao kazi cha Kamisheni ya Tume hiyo ambacho kimefanyika Mkoani Morogoro katika hoteli ya Morena kwa ajili ya kupitia taarifa saba (7) za utafiti uliofanywa hivi karibuni.

Waziri huyo ameeleza kwamba imekuwa ni utaratibu wa kawaida kwa wananchi kupoteza maisha na kupata ulemavu wa kudumu unaosababishwa na ajali za barabarani zinazotokana na makosa yanayoweza kuzuilika hasa kwa mabasi yaendayo masafa marefu.

“Umefika wakati Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania kufanya utafiti na kuja na mapendekezo madhubutiyatakayosaidia kuondoa ajali za barabarani ili kulinda afya na maisha ya watanzania kwa kuwalazimisha wamiliki kuajiri dereva zaidi ya mmoja katika chombo kimoja cha masafa marefu” alisema Waziri

Aidha ameagiza Tumehiyo kushirikiana na wasimamizi wa sheria ya barabaraniili kutafuta suluhisho la kudumu la kuwalinda wasafiri kwa usalama na kuhakikisha wanafika kwa wakati, huku akiligusia swala la bima za maisha katika kuwasidia wathirika.

“Sisi kama wabobevu wa sheria lazima tuangalie kama kampuni inapata ajali za mara kwa mara waachane na biashara ya kusafirisha watu na badala yake wasafirishe mizigo.” alisema

Aidha ameendelea kueleza kwamba Tume ya Kurekebisha sheria kupitia wizara ya katiba na sheria ambao ndio wenye dhamanahazipotayari kuona tayari kuona wananchi wakipoteza maisha kila kukicha.

Aidha, ameitaka Tume ya kurekebisha sheria wasisubiri kuletewa kazi za utafiti au mapitio kama ilivyo sasa na badala yake wafanye kulingana na wanavyoona hali halisi na wanayoyapata wakati wa utafiti.

Hata hivyo Mhe. Waziri aleeza kufarijika kwake na utekelezaji wa mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai yanayofanywa na Tume hiyo ambazo ni Taarifa ya Mapitio ya Mfumo wa Sheria Zinazosimamia Makosa ya Uhujumu Uchumi na Uhalifu wa Kupangwa Nchini; Taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Kifungu cha 91(3) cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai;

Utekelezaji mwingi umekuwa katika Taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Sheria ya Ulinzi wa Mashahidi na Watoa Taarifa;Taarifa ya Mapitio ya Mfumo wa Sheria Zinazosimamia Dhamana; na Taarifa ya Mapitio ya Sheria Zinazosimamia Adhabu ya Viboko Mahakamani na Katika Magereza.

Awali akimkaribisha Waziri huyo Jaji wa Mahakama ya Rufani, Winfrida Beatrice Korosso, ambaye ni Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania, alieleza kwamba Kikao cha Kamisheni ya Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania ni Kikao cha 94 toka Tume hii kuanzishwa ambapo Tume , inatekeleza wajibu wake ipasavyo kwa kuhakikisha vikao vyote vya Kisheria vinafanyika hususan baada ya utafiti na mapitio ya kitaaluma.

Aidha alieleza kwamba Taarifa zilizokamilishwa na Sekretariati, ya Tumebaada ya kufanyika Mapitio, Utafiti na Tathmini katika nyanja mbalimbali za sheria ni Taarifa ya Mapitio ya Mfumo wa Sheria Zinazosimamia Uhujumu Uchumi na Uhalifu wa Kupangwa Nchini na Taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Kifungu cha 91(3) cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai Kuhusu Uondoshaji wa Mashauri Mahakamani.

Pia taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Sheria ya Ulinzi wa Mashahidi na Watoa Taarifa;Taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Sheria Zinazosimamia Usafiri Ardhini; Taarifa ya Mapito ya Mfumo wa Sheria Zinazosimamia Dhamana; Taarifa ya Mapitio ya Sheria Zinazosimamia Adhabu ya Viboko Mahakamani na Magereza;naTaarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Sheria Zinazosimamia Hakimiliki na Hakishiriki.

Mwisho