Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania

Habari

Toeni Maoni Yenu Kwenye Sheria Mbalimbali, Yatafanyiwa Kazi - George Mandepo.


Katibu Mtendaji Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bw. George Mandepo amewataka wadau wa sheria nchini kuwasilisha maoni yao juu ya sheria mbalimbali kwa Serikali kupitia Tume ya Kurekebisha Sheria na Tume itayafanyia kazi kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa.

Bw. Mandepo ameeleza hayo leo tarehe 7 Februari 2024 jijini Dodoma wakati wa kufanyia tathmini ya maoni ya baadhi ya wananchi waliyoyatoa wakati wa maadhimisho ya wiki ya sheria yaliyomalizika tarehe 1 Februari 2024 na kufungwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani ambapo wananchi wengi waliomba Tume ya Kurekebisha Sheria kuwatembelea maeneo yao ili kupata maoni yao kuhusu utekelezaji wa sheria mbalimbali hapa nchini.

Katibu huyo alisema kwamba, Tume ya Kurekebisha imekuwa ikikutana na wadau mbalimbali katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku na wakati wa kufanya utafiti na utoaji wa elimu ya sheria kwa umma ambapo ameeleza kwamba, kupitia utaratibu huo mwananchi mojamoja au vikundi wamekuwa wakipata fursa ya kutuoa maoni yao kwa njia mbalimbali ikiwemo kupitia barua pepe (E-mail), barua ya kawaida, kupiga simu au kuonaa moja kwa moja na Maafisa husika wa Tume ili kueleza changamoto wanazoziona katika sheria zilizopo au mapungufu yoyote kwenye utendaji ambayo wanadhani yanahitaji kuwekewa mfumo wa sheria.

“Tumekuwa tukikutana na wananchi wakati wa utafiti , kutoa elimu kwa umma na wakati wa tathmini lakini bado wananchi wanaweza kutuandikia, kutupigia simu au kutembelea ofisi zetu na kutoa maoni yao na tutatapokea na kuyafanyia kazi kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa”

Aidha, akitolea ufafanuzi swali la mwananchi mmoja aliyeomba Tume itembelee mahabusu na ikiwezekana wanasheria wakakae magererezani kama wafungwa ili waweze kuviona vipengele vya sheria vinavyostahili kubadilishwa (https://youtu.be/7HEO1Amp- yenye kichwa cha habari ‘Nendeni magerezani/Mhabusu huko mtaona vipengele vya kurekebisha”. Bw. Mandepo amesema kuwa, Idara ya Magereza ni moja ya mdau muhimu wa Tume na Magereza ni eneo mojawapo la kupata taarifa za kitafiti zitakazosaidia pia kufanya marekabissho ya sheria kama pia ilivyowahi kupendekezwa na Tume ya Haki Jinai. Alibainisha kuwa, kwa sasa Serikali inafanyia kazi mapendekezo ya mapitio ya sheria mbalimbali zinazosimamia haki ikiwemo zile zinazohusisha haki jinai.