Katibu Mtendaji Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bw. George Mandepo akiwahutubia wadu wakati ukusanyaji wa maoni kuhusu mfumo wa sheria zinazosimamia masuala ya nishati,viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mkutano huo ni hatua mojawapo katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kufuatia maelekezo ya Mhe. Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania kuitaka Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania kwa kushirikiana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kufanya mapitio na maboresho ya sheria ili kuwezesha utekelezaji kamili wa Dira 2050. Mkutano huo wa wadau ulifanyika katika ukumbi wa Hotel ya APC Bunju Mkoani Dar es salaam.