Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania, Jaji mstaafu, January Msoffe ( wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Tume ya kurekebisha Sheria Zanzibar, Khadija Shamte Mzee (wa pili kulia), wakionesha mkataba wa ushirikiano baina Tume ya Tanzania bara na Zanzibar. hafa hiyo imefanyika Julai 12, 2023 jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya kurekebisha sheria bara, Griffin Mwakapeje na kushoto ni Katibu Mtendaji wa Tume ya kurekebisha sheria Zanzibar Musa Kombo.
Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania, Jaji mstaafu, January Msoffe ( wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Tume ya kurekebisha Sheria Zanzibar, Khadija Shamte Mzee (wa pili kulia), wakisaini mkataba wa ushirikiano baina Tume ya Tanzania bara na Zanzibar. hafla hiyo imefanyika Julai 12, 2023 jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya kurekebisha sheria bara Bw. Griffin Mwakapeje kushoto ni Katibu Mtendaji wa Tume ya kurekebisha sheria Zanzibar Musa Kombo
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania mara baada ya kumaliza mazungumzo na watumishi hao wakati wa ziara yake iliyofanyika tarehe 22 Juni, 2023.
Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Mhe. January Msoffe akieleza kwa ufupi historia ya kuundwa kwa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania pamoja na kumkaribisha Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul kwa lengo la kuzungumza na Watumishi wa Tume hiyo wakati wa ziara yake ya kutembelea ofisi hiyo iliyofanyika tarehe 22 Juni, 2023 Jijini Dodoma.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bw. Griffin Mwakapeje akitoa maelezo mafupi yanayohusu Utendaji kazi wa Ofisi ya Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania kwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul wakati wa ziara aliyoifanya kwenye Taasisi hiyo tarehe 22 Juni, 2023 Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul akisalimiana na Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bw. Griffin Mwakapeje pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Mhe. January Msoffe wakati alipowasili kwenye Taasisi hiyo kwa lengo la kuzungumza na watumishi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania mnamo tarehe 22 Juni, 2023 Jijini Dodoma.
Picha ya pamoja ya Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (aliyekaa katikati) akiwa na Majaji wapya wa mahakama ya rufani wakati wa mafunzo yaliyofanyika katika chuo cha IJA Lushoto
Waziri wa Katiba na Sheria Mheshimiwa Damas Ndumbaro alipotembelea banda la Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania,katika siku ya Maadhimisho ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwa ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alipata wasaa wa kutembelea banda la Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania, katika siku ya Kuazimisha miaka mitano tangu kuanzishwa kwa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, tarehe 05 juni, 2023
Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa pamoja na Wakuu wa Mashtaka wa Mikoa wakiwa wanatoa maoni kuhusu tahthmini na utafiti wa sheria zinazohusu makosa dhidi ya Maadili Jana kwenye ukumbi wa NBS jijini Dodoma.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Ndg. Griffin Mwakapeje akitoa ufafanuzi katika kikao cha kukusanya maoni na tathmini ya Sheria dhidi ya makosa ya maadili , kikao hicho kilihudhuriwa na Wakuu wa Wapelelezi wa mikoa pamoja na wakuu wa mashtaka wa mikoa (Hawapo pichani) kutoka Tanzania bara na Visiwani, tarehe 12 na 13 Mei 2023 jijini Dodoma .
Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Jaji Mstaafu January Msoffe(katikati) akiwa ameongoza kikao cha majadiliano ya kukusanya maoni ya tathmini na utafiti wa sheria mbalimbali zinazohusu makosa dhidi ya maadili tarehe 12 Mei 2023 Jijini Dodoma.
Wanasheria wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania wakiwa katika picha ya Pamoja na Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bw. Griffin Mwakapeje, Mara tu baada ya kuhitimishwa kwa Kongamano la Kitaifa la Sheria ya ndoa Tanzania, lililofanyika Ukumbi wa Morena Hotel tarehe 24/04/2023
Baadhi ya Watumishi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Dr. Damas Ndumbaro, katika Ukumbi wa Hotel ya Morena Dodoma
Menejimenti ya Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi Mary Kondo (Katikati waliokaa) mara baada ya uzinduzi wa kikao cha 18 cha Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania, kilichofanyika katika ukumbi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliyopo Njedengwa Dodoma
Bi Moshi J. Muna Mtumishi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Bahi Mh. Godwin Gondwe kipeperushi cha Elimu ya Sheria kwa umma kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania
Katibu mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Ndugu Griffin Venance Mwakapeje, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Natu El-Maamry Mwamba na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Ndugu Emmanuel Mpawe Tutuba wakila Kiapo cha Maadili kwa Viongozi, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 09 Januari, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Moses Mpogole Kusiluka, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Ndugu Emmanuel Mpawe Tutuba, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria Ndugu Griffin Venance Mwakapeje na Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Sivangilwa Mwangesi mara baada ya hafla ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 09 Januari, 2023.