Wananchi mkoani Shinyanga wameshauriwa kusoma masharti y mkataba wa mkopo kabla ya kuchukua mkopo pamoja na kujiridhisha kiwango cha mkopo anachotaka kukopa, riba ya mkopo, kipindi cha muda wa marejesho ya mkopo,pamoja na kujiridhisha kuhusu uhalali wa taasisi ambayo atakwenda kuchukua mkopo husika.
Hayo yameelezwa na Afisa Sheria kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Richard Mdee, mapema leo tarehe 18 Aprili 2026 alipokua akizungumza na wananchi kuhusu sheria, taratibu, kanuni na wajibu wa mkopeshaji na mkopeshaji kupitia kipindi cha asubuhi cha Jumamosi tulivu kilichokua kinarushwa na Redio Faraja iliyopo Manispaa ya Shinyanga.
Wakili Mdee alisema kumekua na changamoto kubwa kwa jamii kutoa malalamiko pindi wanapochukuliwa hatua inapotokea kutofuata makubaliano ya mikopo waliyochukua . Changamoto hii hutokana na baadhi ya wakopaji kutosoma vizuri masharti ya mana wa mkopo ikiwemo kujiridhisha na riba ya mikopo husika na kujikuta wakiingia matatizoni pindi wasipotekeleza matakwa yaliopo katika mkataba.
“unakuta mkopaji anachukua mkopo kisha anaposhindwa kutimiza masharti na kuchukuliwa hatua analalamika hakujua masharti hayo na wakati kwenye mkataba ametia saini kukubali vigezo na masharti vya mkopo, alisema Wakili Mdee.
Aidha aliendelea kwa kusisitiza kwamba ni muhimu wananchi wajiridhishe na masharti ya mkopo ili kupunguza migororo wait w Uwekezaji wa mikopo wanayochukua na iweze kuwasaidia kwenye malengo yao mbalimbali ya kimaendeleo.
Sambamba na hilo Afisa Sheria Bi. Jackilne Nungu alisema kwa mujibu wa sheria mtu binafsi haruhusiwi kukopesha isipokua ataruhusiwa tu kama atafungua kampuni na kuisajili kwa mujibu wa sheria na kutambulika kama tasisi ya kifedha yenye mamlaka ya kukopesha.
Aliendelea kwa kueleza kuwa jamii inapaswa kufahamu kwamba inapotokea mmoja katika familia anataka kukopa na kuweka dhamana (rehani) ya mkopo mali iliyochumwa kwa pamoja ni lazima wote waridhie kwa kushirikishwa juu ya mkataba huo wa mkopo ndipo hatua za mkopo husika ziendelee.
“Ni kosa kwa mali iliyochumwa kwa pamoja mke na mume wakati wa ndoa, na mmoja wa wanandoa kuiweka kama reheni pasipo Tisha ya mwenza wake,alisistiza Bi. Jackline.
Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania inaendelea na zoezi la utoaji wa elimu ya sheria kwa umma kupitia vipindi vya redio, runinga, vikao na wadau ikiwemo wanafunzi wa shule za sekondari na vyuo vya kati ili kuisaidia jamii kujenga uelewa kuhusu masuala ya kisheria.