Government Logo
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania

TUMESHERIA SPORTS CLUB RIADHA SHIMIWI 2026 SIO KINYONGE.
08 Oct 2026
TUMESHERIA SPORTS CL...

Wachezaji wa Tumesheria Sports Club waliowakilisha timu hiyo katika mchezo wa riadha waonesha ushindani mkubwa baada ya mshiriki wa mbio za Wazee Wanawake Mita 100 Bi. Aneth Lyatuu kupata nafasi ya 5 katika kinyang'anyiro hicho kilichowashindanisha manguli wa mbio kutoka wizara, idara na Taasisi mbalimbali za serikali.

Aneth alifanikiwa kushika nafasi hiyo ya 5 katika mashindano yaliyofanyika hivi leo tarehe 2 Octoba 2026 katika Uwanja wa Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro.

Aidha katika mbio za vijana wanaume Mita 100 Mwakilishi wa Tumesheria Zakaria Kegoro yeye alimaliza katika nafasi ya sita.

Michuano ya Shimiwi 2026 inaendelea Moshi mkoani kilimanjaro ambapo inategemewa kuhitimishwa ifikapo Octoba 7, 2026