Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi (DCS) Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania, Bw. Mohamed Mavura, akizungumza na Mkandarasi wa kampuni ya LI JUN DEVELOPMENT CONSTRUCTION CO. LTD anayejenga Jengo la Makao Makuu ya Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT) katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma, mara baada ya kutembelea kuangalia maendeleo ya ujenzi huo tarehe 18 Machi 2025.