Government Logo
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania

WANAWAKE TUMESHERIA NA BUNGE WATOSHANA NGUVU KUVUTA KAMBA MASHINDANO YA SHIMIWI 2025.
04 Sep 2025
WANAWAKE TUMESHERIA...

Timu ya Wanawake Tumesheria Sports Club wamepata sare ya  1-1 na timu ya Wanawake Bunge, katika michuano ya SHIMIWI mchezo wa mzunguko wa tatu wa kuvuta kamba kundi E, Wanawake uliofanyika leo tarehe 4 Septemba 2025 katika Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza.

Tumesheria Sports Club ndio waliokua wa kwanza kupata ushindi katika mtanange huo ambao awamu ya kwanza walifanikiwa kuwavuta Bunge na kuvuna alama 1 huku awamu ya pili Bunge nao wakafanikiwa kuwavuta Tumesheria na kuvuna alama 1 na kufanya mchezo kumalizika kwa kugawana alama 1-1.

Kwa Matokeo hayo kulingana na msimamo wa kundi E kuvuta kamba Wanawake, timu ya Tumesheri na timu ya Bunge zimepata alama sawa kwa timu zote zikiwa na jumla ya alama 5 katika michezo mitatu waliocheza kwa kila timu huku timu ya Uwekezaji wakifuata kwa kuwa na alama 4, timu ya UCSAF wakiwa na alama 2 na Ras pwani wakiwa hawajapa alama katika michezo yote waliyocheza.

Mchezo wa Mwisho katika hatua ya makundi kuvuta kamba Wanawake kwa kundi E utafanyika hapo kesho tarehe 5 Septemba 2025 ambapo timu ya Tumesheria watachuana na timu ya Ras Pwani. 

Tumesheria wametanguliza mguu mmoja mbele kuingia hatua ya 16 bora katika michuano hiyo ikiwa mchezo wao wa kesho tarehe 5 Septemba 2025 watashinda ama kupata sare na wapinzani wao kupoteza kati ya Bunge ama Uwekezaji na ikitokea kufanana alama itawalazimu kuvuta kamba timu zinazofanana alama ili kuwapata washindi watakao ingia hatua ya 16 bora kwakua kila Kundi litaingiza timu 2 hatua  hiyo.