Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania

Habari

TUME YA KUREKEBISHA SHERIA TANZANIA YAZINDUA LAW REFORMER JOURNAL


Naibu katibu mkuu wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Franklin Jasson Rwezimula amepongeza Tume ya kurekebisha Sheria Tanzania kwa kuzindua Law Reformer Journal na kueleza kuwa Journal hiyo itasaidia kuongeza uelewa juu ya mambo mbali mbali ya kisheria.

Dkt. Franklin ameyasema hayo 21 Agosti 2024 katika ukumbi wa Ngorongoro uliopo jengo la Nbs mkoani Dodoma wakati wa Warsha ya kujadiliana umuhimu wa Utafiti katika maboresho ya Sheria nchini iliokwenda Sambamba na Uzinduzi wa Law Reformer Journal ilioandaliwa na Tume hiyo.

Dkt. Franklin ameongeza kuwa Pamoja na kazi kubwa inayofanywa na Tume ya kurekebisha Sheria Tanzania ameutaka Uongozi Wa Tume hiyo kuendelea kufanya Tafiti za Sheria Mbali mbali ili kubaini Sheria zilizopitwa na wakati ziweze kuzifanyia mchakato wa marekebisho ili kuendana na wakati kwa watumiaji.

Ili kuwa na maendeleo endelevu ni lazima tujue je changamoto ni ya upungufu au kuwepo kwa Ombwe la mifumo ya utekelezaji wa Sheria? Ukifanya tafiti itatusaidia kujua na kurekebisha pasipostahili ili kuendana na wakati wa sasa” aliseka Dkt. Franklin

Awali Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Mh. Jaji, Winfrida Korosso alieleza kuwa Mada zilizolengwa kuwasilishwa zinalenga maboresho mbalimbali na Mapendekezo mbali mbali yatakayotolewa kuhusu sheria mbali mbali yatasaidia si tu Tume pekee bali yatasaidia hata katika Maisha kila mmoja.

Korosso aliongeza kwa kusema kuwa kutokana na mabadiliko yanayotokea katika nyanja mbali mbali, tafiti zinazofanyika za kisheria Zinalenga kuendana na mabadiliko ya sayansi na Teknolojia na kufanya Sheria wezeshi ili kuondokana na vikwazo vya kisheria kurahisisha utekelezaji ili kuleta maendeleo ya Nchi.

Kwa upande wake katibu Mtendaji wa Tume ya kurekebisha Sheria Tanzania George Mandepo alisema hapo awali tafsiri ya Sheria zilikua hazigusii madhumuni ya kuanzishwa kwake na kwamba kuanzishwa kwa Tume kulikuja ili kuonazinazingatia Utafiti.

Aidha Mandepo aliongeza kwa kubainisha kua ufanyaji wa Tafiti za kisheria unahusisha maoni ya wadau, Tasisi na Mashirika mbali mbali amba oni sehemu ya watumiaji ili kuweza kufikia dhana ya uwepo wa sheria inayoendana na wakati na inayoeleweka kwa watumiaji.

Sisi kama Tume ya kurekebisha Sheria tutaendelea kuishauri serikali na kushirikiana na wadau mbali mbali katika kuhakikisha tunafanya utafiti na kupokea maoni ili kubadilisha sheria ziweze kuendana na wakati” alihitimisha Mandepo.