Tume ya Kurekebisha sheria Tanzania imejivunia kupunguza kwa kiasi kikubwa migogoro inayohusiana na ardhi, mirathi na ndoa, kupitia mapitio ya sheria, tafiti na elimu ya sheria kwa umma ambayo imekuwa ikitolewa katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
Maelezo hayo yametolewa leo tarehe 24.07.2025 na Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Bw. George Mandepo wakati akieleza mafanikio ambayo yamefikiwa naTume hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja wa 2024/25, maelezo aliyoyatoa akiwa katika kipindi cha redio cha Jilawi cha TBC Jamii Mkoani Dodoma.
Mandepo amesema, tume imekuwa ikishiriki kikamilifu katika kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia (Samia Legal Aid) ambayo imetolewa nchi nzima chini ya Wizara ya Katiba na Sheria ambapo mawakili wa serikali walitoa elimu kwa wananchi kuhusiana na namna ya kutatua changamoto ya migogoro ya namna hiyo.
“Tume ya Kurekebisha Sheria tumekuwa tukishiriki kwa kiasi kikubwa katika kutoa elimu ya sheria kwa umma kupitia kampeni ya msaada wa kisheria wa Mama Samia, hii inatupa faraja kwakuwa migororo ya ardhi,mirathi na Ndoa imeendelea kupungua kutokana na elimu inayotolewa” Alisema Mandepo.
Hata hivyo Tume imekuwa ikikutana na wadau mara kwa mara ikiwemo kwenye maonesho ya sabasaba, Nanenane Wiki ya sheria na kwenye makongamano mbalimbali ambapo changamoto mbalimbali za mirathi, ndoa na migogoro ya ardhi ilitatuliwa alieleza Mandepo.
“migogoro ya ardhi imekuwa chanzo kikuu cha migogoro ya kijamii nchini Tanzania, hasa vijijini na mijini. Ili kukabiliana na hilo, Tume ilifanya utafiti maalum kuhusu sheria za ardhi, ambapo walibaini kuwa kulikuwa na tatizo la umilikaji mara mbili (double allocation) na sasa sheria hilo” alisema Mandepo
Aidha Katibu mtendaji aliendelea kubainisha kwamba tume imefanikiwa kutoa elimu kuhusu mirathi na Ndoa kupitia vipeperushi majarida na wakati wa vikao vya wadau na kupitia njia mbalimbali za redio na Runinga lengo likiwa ni kuendelea kupunguza migogoro ya aina hiyo kwenye jamii kupitia marekebisho ya sheria
"Tunataka kumaliza kabisa tatizo la umiliki mara mbili wa ardhi ambalo limekuwa likisababisha mapigano, chuki na umaskini kwa wananchi” alisema Katibu Mtendaji wa Tume, George Mandepo.