Government Logo
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania

KATIBU MTENDAJI TUME YA KUREKEBISHA SHERIA TANZANIA AWATAKA WAKUU WA VITENGO NA IDARA KUFAHAMU MCHAKATO WA KIBAJETI.
19 Nov 2025
KATIBU MTENDAJI TUME...

Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria, Bw. George Mandepo, ametoa wito kwa wakuu wa vitengo na maafisa bajeti kuhakikisha wanauelewa wa kina kuhusu mchakato wa kuandaa na kutekeleza bajeti katika idara zao, ili kuboresha utendaji kazi na matumizi sahihi ya rasilimali za umma.

Akizungumza wakati wa kufunga kikao cha baraza la wafanya kazi lililofanyika leo. tarehe 19.11.2025 Bw. Mandepo alisema kuwa changamoto nyingi zinazojitokeza katika utekelezaji wa bajeti zinatokana na kutokuelewa kwa kina hatua muhimu za upangaji, usimamizi na ufuatiliaji wa bajeti.        

“Ni muhimu kila mkuu wa kitengo/Idara na maafisa bajeti kufahamu kwa undani mzunguko mzima wa bajeti — kuanzia maandalizi, utekelezaji, hadi tathmini. Hii itasaidia kuongeza ufanisi, kuondoa upotevu wa rasilimali na kuboresha utoaji wa huduma kwa umma,” alisema Mandepo.

Aidha, Bw. Mandepo alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya vitengo mbalimbali ndani ya tume hiyo ili kuhakikisha kuwa bajeti inayoandaliwa inalingana na mahitaji halisi ya taasisi na inaleta matokeo yanayotarajiwa.

Bw. Mandepo aliongeza kuwa tume inaendelea kuchukua hatua za ndani za kuboresha ujuzi wa watumishi wake kupitia mafunzo na semina ili kuwajengea uwezo katika masuala ya bajeti, usimamizi wa fedha na utekelezaji wa miradi.

Alihitimisha kwa kusisitiza kuwa uwajibikaji na uadilifu ni misingi muhimu katika matumizi ya bajeti, na kuwataka maofisa wote kufuata kanuni na taratibu zinazoongoza matumizi ya fedha za umma.