Government Logo
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania

Katibu Mtendaji aongoza kikao cha Menejimenti– Tume ya Kurekebisha Sheria
23 Oct 2025
Katibu Mtendaji aong...

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania jana tarehe 23/10/2025 imefanya kikao cha Menejimenti kilichoongozwa na Katibu Mtendaji wa Tume hiyo, Bw. George Mandepo katika ukumbi wa mikutano wa Tume hiyo uliopo  Jijini Dodoma.

Kikao hicho kililenga kupitia utekelezaji wa mipango ya Tume kwa kipindi cha robo  mwaka pamoja na kupanga mikakati ya kuimarisha utekelezaji wa majukumu yake kwa kipindi kijacho.

Akifungua kikao hicho, Katibu Mtendaji alisisitiza umuhimu wa ushirikiano baina ya watumishi na Menejimenti ili kuongeza  uwajibikaji na ubunifu katika kutekeleza majukumu ya Taasisi.

“Ushirikiano baina ya watumishi pamoja na kufanyika kwa vikao vya Idara/Vitengo kwa wakati kutasaidia kuondoa malalamiko na kuongeza uwajibikaji kwa watumishi” alisema Mandepo

Katika kikao hicho, mawasilisho mbalimbali yalitolewa kwa baadhi ya  wakuu wa Idara yakionesha mafanikio katika utekelezaji wa majukumu ya Taasisi hiyo yakiwemo taarifa ya utekelezaji wa majukumu katika kipindi cha robo mwaka, miradi  ya utafiti inayoendelea na hatua mbalimbali zilizofikiwa katika uboreshaji wa sheria ya Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania.

Kikao hicho kilihitimishwa kwa maazimio kadhaa, yakiwemo kuimarisha mifumo ukiwepo ule wa kukusanya maoni ya wadau, mafunzo kwa watumishi wa Tume, kuboresha mifumo ya taarifa na kuhakikisha upatikanaji wa rasilimali stahiki kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu ya msingi ya Tume.