Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania

Miradi Inayoendelea

Mapitio ya Mfumo wa Sheria Zinazosimamia Wazee wa Mahakama


Mapitio ya Mfumo wa Sheria Zinazosimamia Wazee wa Mahakama Tanzania

Mapitio ya Mfumo wa Sheria Zinazosimamia Wazee wa Mahakama ni mradi ulioanzishwa na Tume. Mradi huu ni miongoni mwa miradi iliyoainishwa kwa ajili ya mapitio kufikia mwaka 2023 katika Mpango Mkakati wa Muda wa Kati wa Tume wa Miaka mitano ulionza mwaka wa fedhawa 2018/19 hadi 2022/23.

Mpango Mkakati unalengo la kufikia lengo kuu la Tume ambalo ni kuboresha utawala wa sheriaambao unahimiza kukuza mazingira mazuri yatakayoipeleka Tanzania katika kukuza viwanda vya kati kufikia 2025 kulingana na Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2025.

Utafiti huu unalengo la kupitia mfumo wa sheria zinazosimamia wazee wa mahakama nchini Tanzania ili kuainisha upungufu na kisha kutoa mapendekezo yenye lengo la kuhakikisha utoaji haki unakuwa wa ufanisi na wa haraka.

Utafiti huu pia unalengo la kuondoa changamoto zilizojitokeza katika vipengele vinavyohusiana na vigezo, uteuzi, wajibu na muda wa kutumikia uzee wa baraza.Hivyo, utafiti huu utapendekeza hatua madhubuti zitakazoweza kutatua changamoto zinazoukabili mfumo wa sheria unaosimamia wazee wa baraza.