Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania

Miradi Inayoendelea

Mapitio ya Mfumo wa Sheria Zinazosimamia Masoko ya Kilimo Tanzania


Mapitio ya Mfumo wa Sheria Zinazosimamia Masoko ya Kilimo Tanzania


Katika mwaka wa fedha 2020/2021 Tume inafanya Mapitio ya Mfumo wa Sheria Zinazosimia Masoko ya Mazao ya Kilimo Tanzania. Mapitio haya yanafanywa na Tume kulingana na Mpango Mkakati wa Muda wa Kati wa Tume wa Miaka Mitano ulionza mwaka wa fedhawa 2018/19 hadi 2022/23.

Mapitio haya yanahusisha sheria zilizoainishwa katika Mpango Mkakati wa Tume wa Kati wa Kipindi cha Miaka Mitano unaotekelezwa hadi kufikia mwaka 2023 ili kufikia lengo kuu la Tume ambalo ni kuwa na utawala bora wa kisheria ambao unahimiza ukuaji wa viwanda vya kati.

Lengo kuu la kufanya mapitio ni kuwa na mfumo jumuisha naunaoweza kuratibiwa kwa urahisi kwa ajili ya masoko ya mazao ya kilimo; kuweka mfumo wa haki, ushindani na mfumo wa masoko endelevu; kuboresha miundo mbinu ya masoko nanamna ya usimamizi wa hatari katika masoko ya mazao.