Miradi Inayoendelea
(a) Mapitio ya Sheria ya Takwimu Sura ya 351
Tume ya Kurekebisha Sheria inafanya Mapitio ya Sheria ya Takwimu, Sura ya 351. Mapitio haya yanalenga kuboresha Mfumo wa uratibu na kurahisisha upatikanaji wa takwimu katika Kanzidata ya Taifa. Taarifa ya Mapitio itabainisha changamoto zilizopo na kutoa mapendekezo ya namna ya kukabiliana nazo.