Habari
WATUMISHI WA TUME YA KUREKEBISHA SHERIA TANZANIA WASHIRIKI SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
Tarehe 8 Machi, 2023, Wanawake Watumishi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT) wameungana na wanawake wengine kote Duniani katika Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Wanawake Duniani. Katika Mkoa wa Dodoma, maadhimisho hayo yalifanyika katika Viwanja vya Sabasaba Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma, yakiwa na Kaulimbiu
"UBUNIFU NA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA CHACHU KATIKA KULETA USAWA WA KIJINSIA."