Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania

Habari

Watumishi LRCT Watakiwa Kulinda Rasilimali kwa Maendeleo


Watumishi wa Tume ya kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT) wametakiwa kuzilinda na kutunza Rasilimali zilizopo chini ya Taasisi hiyo kwa kuwa ndizo zitakazo saidia kuyafikia malengo waliyojiwekea.

Akiongea wakati wa kikao cha menejimenti ya Taasisi hiyo kilichofanyika Desemba 4, 2023, katika moja ya kumbi wa mikutano wa ofisi hiyo, Kaimu Katibu Mtendaji Burhani Kishenyi amesema watumishi wanatakiwa kuzilinda na kuzitunza rasilimali zilizopo ikiwemo, rasililimali fedha, watu, na rasilimali muda kwa kuwa ndio vitu muhimu katika kuyafikia malengo waliojiwekea kupitia kazi za kila siku wanazozitekeleza.

wapo watumishi ambao wanaacha feni na taa zikiwa zinawaka masaa yote ya kazi, kuanzia juma tatu hadi juma pili bila kuzimwa jambo ambalo linaongeza gharama za uendeshaji hii sio sawa lazima kila mtu awe makini na ofisi yake , ofisi ya utumishi na rasilimali watu waonyeni na ikibidi warudisheni watako acha taa au feni zikiwaka ofisini kwao hata kama ni muda usiokuwa wa kazi”Kishenyi .

Aidha ameagiza kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa watumishi watakaobainika kutumia rasilimali vibaya ikiwemo ofisi, magari na muda na ikiwemo kuwarudisha ofini kuzima taa au feni watakao bainika kuacha ofisi za katika mazingira hayo hata kama ni siku au muda usikuwa wa kazi.