Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania

Habari

UONGOZI WA TUME YA KUREKEBISHA SHERIA TANZANIA WAKUTANA NA UONGOZI WA SEKRETARIETI YA CHAMA CHA MAWAKILI TANGANYIKA (TLS)


Viongozi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT) wakutana na kufanya kikao cha pamoja na Uongozi wa chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) . Kikao hicho kilifanyika katika Ofisi za Tume ya Kurekebisha Sheria zilizopo Chuo Kikuu cha Dodoma.Lengo la kikao hicho ni kuutambulisha Uongozi mpya wa TLS na kubadilishana mawazo ili kuimarisha ushirikiano katika kufanya maboresho ya sheria nchini. Katika kikao hicho, Tume imeahidi kuendelea kushirikiana na TLS katika utafiti na mapitio ya Sheria kwa lengo la kuhakikisha Sheria zilizopo zinapitiwa nakuhuishwa ili kuendana na wakati, Tume iliwakishwa na Mhe. Jaji Mstaafu January Msoffe ambaye ni Mwenyekiti wa Tume;Bw. Griffin V.Mwakapeje Katibu Mtendaji wa Tume; Bi. Zainabu I. Chanzi Kaimu NaibuKatibu wa Kitengo cha Elimu ya Sheria kwa umma na Dkt. Kalekwa Kasanga Afisa Sheria Mwandamizi. Aidha, TLS iliwakishwa na Bi. Mariam Othman Kaimu Mtendaji Mkuu, Bw. Kaleb Gamaya Mtendaji Mkuu Mstaafu na Bi. Mercy Kessy Mwakilishi wa TLS, Dodoma.