Habari
Tume yakabidhi Ripoti ya Mapitio ya Sheria za sheria zinazosimamia Migogoro ya Ardhi kwa Waziri wa Katiba na Sheria
Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania yakabidhi Ripoti ya Mapitio ya Sheria za sheria zinazosimamia Migogoro ya Ardhi kwa Waziri wa Katiba na Sheria. Mwenyekiti wa Tume akikabidhi Ripoti hizo alisema Tume ilikusanya maoni katika mikoa ya Arusha, Mwanza , Morogoro, Mbeya, Iringa, Dar es Salaam na Dodoma kwa wadau mbalimbali kwa lengo la kupata maoni ya wadau na kisha kuchambua maoni hayo na kupendekeza njia nzuri ya utatuzi wa migogoro ya ardhi