Government Logo
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania

TUME YA KUREKEBISHA SHERIA TANZANIA YASHIRIKI MAONESHO YA 50 YA KIMATAIFA YA BIASHARA (SABASABA) 2026.
30 Jun 2026
TUME YA KUREKEBISHA...

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania inashiriki katika Maadhimisho ya Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yaliyoanza kufanyika tarehe 28 Juni hadi 13 Julai 2026 katika viwanja vya Sabasaba, Jijini Dar es Salaam.

Maadhimisho hayo yamekutanisha kampuni na taasisi mbalimbali za biashara na huduma zilizo za Serikali na binafsi ili kuwasogezea huduma wananchi ambapo mwaka huu yamebeba kaulimbiu isemayo “Kuchochea Uwajibikaji Jumuishi kwa Huduma Endelevu”, ikiwa ni msisitizo wa kuimarisha uwazi, uwajibikaji na ubora wa huduma za umma nchini.

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania inatumia nafasi hiyo ili kuelimisha umma kuhusu majukumu yake ya msingi ya Mapitio, Tathmini, na Utafiti juu ya maboresho ya sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili ziendane na mahitaji ya sasa ya kijamii, kiuchumi, kiteknolojia na kuwezesha kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Katika hatua hiyo Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania itatumia Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba kama fursa muhimu ya kusikiliza maoni ya wananchi, hasa kuhusu changamoto za kisheria zinazowakabili na mapendekezo ya maboresho ya sheria.