Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania

Habari

TUME YA KUREKEBISHA SHERIA TANZANIA YAKUTANA NA WADAU KUJADILI MABORESHO YA SHERIA YA KAMPUNI NA MABORESHO YA SHERIA YA USAJILI WA MAJINA YA BIASHARA


Tume ya kurekebisha Shheria Tanzania Imekutana na wadau kujadili Maboresho ya sheria ya Makampuni ya sura namba 212 na sheria ya usajili ya majina ya Biashara sura namba 213 ili kubainisha changamoto na mapungufu yaliopo katika sheria hizo ambayo yanaweza kuathiri utekelezaji wake na kupendekeza maboresho ya kutatua changamoto na kuondoa mapungufu.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa kikao hicho cha majadiliano tarehe 11 Machi 2024 Mkoani Dar es salaam akimwakilisha katibu mkuu wizara ya Viwanda na Biashara, Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Ushindani Willium Erio alisema kuboreshwa kwa sheria ya kampuni na sheria ya Majina ya Biashara kulingana na mazingira ya sasa ya kiuchumi na uendeshaji wa biashara kutasaidia kufikia malengo ya serikali mwelekeo wake wa kuwa na Uchumi wa kidigitali.

Aidha Erio alieza kuwa dira ya maendeleo ya Taifa ya Mwaka 2000-2025 inahitaji kuwa na Uchumi imara wa kuweza kukabiliana na ushindani na kutanabaisha kuwa mabadiliko ya sheria hizo yatasaidia kuongeza kuboresha mazingira mazuri ya biashara ambayo yatavutia zaidi wawekezaji kuwekeza Tanzania.

“Kwahiyo ni dhahiri kabisa hiki kinachofanyika ni nia itakayotupeleka katika sehemu sahihi” alisisitiza Erio.

Kwa upande wake katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania George Nathaniel Mandepo,alisema Pamoja na kuendelea kwa mchakato huo wa majadiliano juu ya maboresho ya sheria ya Makampuni na sheria ya Majina ya Biashara,pia Tume hiyo imekua ikifanya mapitio juu ya sheria mbali mbali ili kutengenza mazingira mazuri ya Uwekezaji Nchini.

“tunaendelea na wadau kukusanya maoni yao na kuwasikiliza ambapo wadau wengi wanaona kuwa na sheria ya makapuni ambayo itakuwa wezeshi isiwe inazuwia kufanyika kwa shughuli za kibiashara” alieleza Mandepo alipokua akitoa baadhi ya maoni ya mfano inayopendekezwa na Wadau wa kikao hicho cha Majadiliano.

Kwa mujibu wa Isdory Nkindi Mkurugenzi wa usajili wa Makampuni na Majina ya Biashara wa wakala na Leseni (BRELA) alisema utafiti wao wa ndani ulibaini sheria hizo kuwaacha nyuma kutokana na masuala ya kisayansi na kiteknolojia akitolea mfano wa kuwapo kwa baadhi ya makampuni yaliopo nje ya Tanzania kushindwa kufika Tanzania kuwekeza na hivyo kuona kuna kila sababu ya kufanyiwa mabadiliko.

“Utafiti wetu wa ndani tulibaini kwamba kidogo sheria hizi zinatuacha nyuma kulingana na maendeleo ya sayansi na teknoloji” alisema Isdory