Habari
Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT) imetoa elimu kuhusu dhana ya mapato yatokanayo na uhalifu, ambayo inahusu mali, fedha, au faida zinazopatikana kutokana na vitendo vya kihalifu. W
Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT) imetoa elimu kuhusu dhana ya mapato yatokanayo na uhalifu, ambayo inahusu mali, fedha, au faida zinazopatikana kutokana na vitendo vya kihalifu.
Wakitoa mada hiyo katika kituo cha redio cha Banana Fm na Redio five ya Mkoani moshi na Arusha Mawakili wa Serikali Anjela Mnzava Shila na Vicky Mbunde kutoka Tume hiyo wamesema lengo la elimu hiyo ni kuhakikisha jamii inaelewa kuwa mali zote zinazopatikana kupitia njia zisizo halali zinaweza kuchukuliwa na serikali kupitia taratibu za kisheria ili kudhibiti uhalifu na kupunguza motisha kwa wananchi wa kushiriki katika vitendo vya kihalifu.
Wakili wa serikali Anjela Shilla akielezea maana ya mapato ya uhalifu alisema ni mapato au mali yoyote itokanayo na uhalifu ambapo alibainisha kwamba suala la mapato yatokanayo na uhalifu ni mtambuka kwa kuwa linalogusa sheria mbalimbali kama vile Sheria ya Mapato yatokanayo na uhalifu, Sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa , Sheria ya kuzuia utakasishaji wa fedha haramu, Sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya, Sheria ya Wanyamapori, na Sheria ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu. Sheria hizi zimeelezea namna ya utaifishaji wa mali zitokanazo na uhalifu kwa Nia ya kuzuia uhalifu na kufundisha jamii kuwa uhalifu haulipi.
Aidha Shila ameeleza kwamba elimu hiyo inahusisha kuwaelimisha wananchi na taasisi za fedha juu ya mbinu zinazotumika kuficha mazao ya uhalifu, kama vile utakatishaji wa fedha, na umuhimu wa kutoa taarifa wanapoona shughuli za kutiliwa shaka.
Kwa upande wake Wakili Vicky Mbunde amefafanua kwamba zipo sheria ambazo zinazohusika na kusimamia mapato yatokanayo na uhalifu ambazo zinalenga kudhibiti, kuchunguza, na kutaifisha mali au fedha zinazopatikana kupitia vitendo vya kihalifu.
Tanzania kama nchi mwanachama wa mikataba mbalimbali ya nje ya nchi imesaini Mkataba wa Umoja wa Mataifa Dhidi ya Uhalifu wa Kupangwa Unaovuka Mipaka na Mkataba wa Umoja wa Mataifa Dhidi ya Rushwa unaotaka nchi wanachama kuweka Mifumo dhabiti ya kisheria ya Kupambana na Uhalifu