Habari
NAIBU WAZIRI JUMANNE SAGINI APONGEZA KAZI ZA TUME YA KUREKEBISHA SHERIA TANZANIA
Naibu Waziri Wizara ya Katiba na Sheria Mhe,JumanneSagini ameipongeza Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT) kwa kile kinachotajwa kwamba Sheria wanazozifanyia utafiti zinadumu kwa muda mrefu bila ya kuhitaji mabadiliko.
Pongezi hizo amezitoa leotarehe 8/5/2024alipotembelea ofisi za Tume hiyozilizopo katika majengo ya chuo Kikuu Cha Dodoma ambapo alizungumza na watumishi wa Tume ya kurekebisha sheria na pamoja na watumishi wa ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ambapo amesema Sheria zilizofanyiwa utafiti na Tume hiyo zinadumu kwa muda mrefu kwa kuwa Zinahusiha utafiti wa kina kwa wadau mbalimbali.
" Zipo Sheria ambazo zilitungwa bungeni ikiwemo Sheria ya Tozo ambapo baada ya miaka miliwili tuiifanyia marekebisho, hii inamaanisha kwamba Sheria zinazohitaji marekebisho ya muda mfupi hazikufanyiwa utafiti wa kutosha, nawapongeza kwa jitihada zenu za kufanya mapitio na utafiti wa kina." alisema Sagini.
Aidha Mhe. Sagini ameiagiza Tume kuimarisha uhusiano wake na wizara zotepamoja na Taasisiili ziweze kuwatumia wanapotakaSheria mpya au maboresho ya sheria zao, huku akisisitiza tume hiyo kuwa Proactive katika kuzisifika kazi za taasisi nyingine.
“Tume hii inatakiwa kuwaproactive kwa kuzipitia sera mbalimbali ambazo zipo katika hatua za kubadilishwa, Sheria zinazorudishwa na bunge mzifanyieutafiti” alisema Sagini
Aidha ameikumbusha Tume hiyo kujenga tabia ya kuzifuata kazi zilipo badala ya kuzisubiri ziletwe kwa kuwakufanya hivyo kunaongeza utungwaji wa sheria ambazo haukidhi Mahitaji ya muda mrefu.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na SheriaDkt. Khatibu Kazungu ameitaka Tume kuhakikisha idadi ya wanasheria inaongezeka kufikia asilimia 50% ya watumishi wa Tume hiyo ili kurahisisha utekelezaji wa majuku ya yao
Katibu Mkuu ameendelea kusema kwamba kwa sasa ni muhimu Tumeinatakiwa kuongeza ushirikiano baina yake na vyuo vikuu vinavyotoa michepuo ya sheria ili kuimarisha taaluma ya utafiti wa sheria kupitia vyuo hivyo.
Hata hivyo Katibu Mkuu amesisitiza Taasisi hiyo kutumia wachumi wake pamoja na wa wizara ya Katiba na Sheria kuandaa maandiko ya kuomba fedhakwa ajili ya kazi za maendeleo ili kupunguza changamoto zinazokabili Taasisi hiyo.
Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Tume ya kurekebisha sheria Tanzania Katibu Mtendaji George Mandepo amesema kwa sasa tayari Tume imashakamilisha miradi miwili (2) ambayo ni tathmini ya sheria zinazosimamia haki miliki na haki shirikipamoja na mapitio ya sheria zinazosimamia makosa ya kupangwa na uhujumu uchumi.