Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania

Habari

​Mangula Awasihi LRCT Kufanya kazi Kizalendo.


Mangula Awasihi LRCT Kufanya kazi Kizalendo.

Watumishi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania wametakiwa kufanya kazi kwa uzalendo katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ili kuongeza ufanisi katika kuwahudumia wananchi.

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 17/04/2024 na Makumu Mwenyekiti Mstaafu Chama cha Mapinduzi Bw. Philip Mangula alipokuwa akitoa mada kuhusu uzalendo na utaifa iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Shule ya Uongozi cha Mwl. Nyerere iliopo Kibaha Mkoani Pwani.

Bw. Mangula alisema elimu ya uzalendo ni muhimu kwa watumishi wote kwa kuwa inabadilisha utendaji kazi katika utumishi wa umma na kukamilisha lengo la serikali la kupeleka huduma stahiki kwa wananchi.

“Kila mtumishi anapaswa kuwa na moyo wa uzalendo katika kujenga nchi, Taifa hili uzalendo ndio uliondoa ukabila na kujenga umoja wa kitaifa”alisema Mangula.

Aidha amesema uzalendo unamfanya mtumishi kufanya kazi kwa kujitolea kwa hali na mali katika kuitumikia serikali na wananchi.