Habari
MAKAMU WA RAIS AFUNGA RASMI MAADHIMISHO YA NNE YA SIDO MKOANI NJOMBE
Taasisi 30 za Serikali na Sekta binafsizilizoshiriki Maadhimisho yaNne yaliyoandaliwa na Shirika lakuhudumia viwanda vidogo (SIDO)kushiriki kwa nafasi zao Katika uzalishaji wa vifungashio nakutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazokabiliSekta ya viwanda vidogo na vya Katihapa Nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo tarehe28.10.2023 na Makamu wa Ras wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Isdori Mpango wakati wa kufunga maadhimisho hayo yaliyoadhimishwa Katika uwanja wa sabasaba Mkoani njombe baada ya kudumu kwa Siku Sita (6) tokea tarehe 23 yalipofunguliwa.
Makamu wa Rais amesema sekta ya viwanda vidogo na vya Kati Ina mchango mkubwa Katika ukuaji wa uchumi wa nchi hivyo ni muhimu taasisi zisaidie upatikanaji wa mitaji, mazingira mazuri ya biashara , elimu ya ujasiriamali na Sheria mbalimbali zitakazosaidia kupiga hatua mbele.
"Nimetembelea mabanda na nimeona teknolojia mbalimbali za usindikaji na kilimo na nimeskia changamoto mbali mbali zinazokabili Sekta ya viwanda vidogo, hivyo niagize taasisi zote zilizopo hapa kuhakikisha kila moja inatafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili wajasiriamali"
Aidha Makamu wa Rais ameelekeza Taasisi ya ubora na viwango (TBS) kuhakikisha inawafikia wajasiriamali wadogo ili kuzipatia ubora bidhaa zao huku akizipongeza benki za CRDB, Azania Benki naTADB kwa kupunguza riba kwa wajasiriali wadogo na wakulima.
Hata hivyo, Makamu wa Rais ameagiza gharama zateknolojia za bidhaa zinazotengenezwa na SIDOziweze kupatikana kwa bei nafuu ili ziweze kununuliwa na wajasiriamali wadogo na wakati na zipatikane sehemu mbalimbali Nchini.
Awali Mkuu wa Mkoa huo Antony Mtaka amesema maonesho hayo yamehusisha wajasiriamali 628 Kati ya 800 waliokuwa wametakiwa na Taasisi 30 za Serikali na Sekta Binafsi.