Habari
JAMII YAASWA KUZINGATIA HAKI NA WAJIBU KABLA YA KUSAINI MIKATABA.
Jamii inapaswa kuzingatia uhakika wa utekelezaji wa mkataba kabla ya kuingia katika makubaliano yenye nguvu kisheria.
Hayo yameelezwa na Jackline Nungu amba ni Afisa sheria kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Octoba 31,2024 alipokua anazungumza katika kipindi cha Breakfast Boat kupitia Redio VOS FM Mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.
Akitoa elimu ya sheria juu ya mikataba Jackline aliasa jamii kuhakikisha inapotokea wanafanya makubaliano ya aina yoyote yenye sura ya mkataba ni vema kila mmoja akahakiki dhima ya makubalino yaliomo kama anaweza kuyatekeleza ili kuepuka kuhisi kuonewa pindi inapotokea kuchukuliwa hatua kwa kutotekelezwa kwa mujibu wa makubaliano husika.
“Kabla haujasaini mkataba hakikisha yale majukumu unaweza kuyatekeleza na hata kama ipo katika lugha ya kigeni una haki ya kuomba utafsiriwe ili ujue wajibu na haki zako kwa mujibu wa mkataba” alisema Jackline.
Aidha Jackline alieendelea kueleza ijapokua kuna aina mbili za mkataba Maandishi na Maneno lakini alihimiza jamii kupendelea kutumia mkataba wa maandishi kwakua ni rahisi kuthibitisha hata mahakamani pindi mkataba husika unapokiukwa kwakua unakua katika kumbukumbu ya kuonekana na wahusika kua wameweka Saini zao wakati wa makubaliano.
Awali Naibu katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Zanab Chanzi alileza ni vema jamii ikafahamu kuwa mkataba ni makubaliano halali yenye nguvu kisheria yanayofungabpande mbili kisheria kutekeleza haki na wajibu wao kwa mujibu wa mkataba husika, hii ni kwa mujibu wa sheria ya mkataba Sura ya 345. Zainab alisema kunapokua na mkataba na ukaenda sawa sawa katika kutekelezwa huwa ni shwari ila inapotokea changamoto, pande ambayo inahisi hakinyake imevunjwa hutakiwa kuthibitishia mahakama kama kweli kulikua na makubaliano hayo hususan katika mkataba wa maneno.
“Mahakama kabka ya kutoa maamuzi itazingatia mahusiano ya pande mbili za mkataba, mwenendo wa mahusiano hayo kabla, wakati na baada ya kuingia katika makubaliano ili kuhakikisha haki imetendeka. “Muhimu sana katika mikataba kuwe na uwazi na uelewa baina ya pande zote mbili” alisema Zainab Katika hatua hiyo Zainab
Aliongeza kwa kubainisha inapotokea wahusika wanatia Saini katika mkataba husika maana yake wamekubaliana na kilichoandikwa na kwamba ikitokea kutotekelezwa hakutakua na kisingizio cha kukwepa kuwajibika kwa kukiuka makubaliano husika.
“Kwa mujibu wa sheria mkataba wowote unatakiwa kuwa na malipo halaliambayo yanakubalika na kwamba malipo hayo yanaweza kuwa fedha,mali au kitu chochote” aliongeza kwa kueleza Zainab
Inaelezwa kuwa sheria imebainisha muda wa kufungua shauri baada ya mkataba kuvunjika kuwa ni miaka sita kwa mujibu wa Sheria ya ukomo, Sura ya 89 ya Sheria za Tanzania na kwamba muda huo huanza kuhesabiwa pale mkataba unapovunjika. Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania inaendelea na zoezi la utoji wa elimu kwa Umma katika mkoa wa Rukwa kupitia vyombo vya Habari ikiwamo redio ikiwa ni sehemu ya kutekeleza majukumu yake.