Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania

Habari

Elimu Ya Sheria Ya “Plea Bargaining" Ilivyofungua Vichwa Vya Wakazi Wa Mkoa wa Arusha


Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT) imefanya ziara katika Mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro kwa lengo la kutoa elimu ya sheria mbalimbali kwa wananchi

Ziara hiyo ilibainisha kwamba Sheria ya “plea bargaining” imeleta mwamko mkubwa miongoni mwa wakazi wa Mkoa wa Arusha na kwingineko Tanzania kutokana na manufaa yake ya kupunguza muda wa kesi, gharama za uendeshaji wa mashauri, na hata kuepuka msongamano katika magereza.

Hayo ni baadhi mambo ambayo wananchi mkoani Arusha walizungumza kwa njia ya simu na ujumbe mfupi wa maneno katika kituo cha Redio cha TBC na Savvy Fm wakati Wanasheria wa Tume hiyo Vick Mbunde na Anjela Shila wakitoa elimu ya sheria kuhusu kupunguziwa adhabu kwa kukiri kosa.

Awali akifafanua kuhusu sheria hiyo Wakili wa Serikali Vicky Mbunde alisema kwamba Plea bargaining, inayojulikana pia kama makubaliano ya kukiri kosa kwa makubaliano maalum, sheria ambayo ilianza kutumika rasmi Tanzania kupitia mabadiliko ya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) ya mwaka 2019, na imekuwa ikihamasishwa kwa nguvu katika mfumo wa sheria.

“mtuhumiwa anapokiri kosa mbele ya muendesha mashtaka , anaweza kupunguziwa adhabu baada yay a mahakama kujiriidhisha na alichokiri . Huu ni utaratibu unaotambuliwa kisheria kama "plea bargaining" ambapo mahakama inaweza kuzingatia kukiri huku kama sababu ya kupunguza adhabu”. Alisema Wakili Vicky Mbunde.

Katika kipindi hicho ambacho wananchi wengi walipiga simu na kutuma ujumbe ,fupi waliuliza idadi kubwa ya maswali huku wakitwataka mawakili hao wa serikali kufafanua umuhimu wa kukikri kosa kwa m,mtuhumiwa na upande wa serikali.

Akijibu maswali hayo wakili Anjela Shila alifafanua kwamba sheria ya Plea Bargaining ina umuhimu mkubwa kwa wananchi na Serikali kwa ujumla kwa sababu inaharakisha Utaratibu wa Kesi Mahakamani kutokana na idadi kubwa ya kesi zinazojazana kwenye Mahakama za ngazi tofauti hivyo , mfumo wa plea bargaining umeonekana kuwa mkombozi kwa kuwa unaruhusu kesi kumalizwa haraka bila kupitia mchakato mrefu wa usikilizaji.

Hata hivyo Wakili Anjela amefafanua kwamba mfumo huo unasaidia kupunguza Msongamano wa Magereza kwa maana kwamba kuna nafasi ya kuangalia mashauri yao kwa mtazamo mpya, wakati mwingine kupokea adhabu nyepesi kwa kukiri mapema na kupunguza athari za kifungo kirefu bila ulazima ambapo alieleza kwamba mfumo huu pia unahimiza wahusika kubadilika na kujifunza kutoka kwenye makosa bila adhabu kali zisizo za lazima.

Aidha alieleza kwamba mfumo huo unasaidia kukuza Uwajibikaji na Haki ambapo Kupitia plea bargaining, mahakama na waendesha mashitaka wanaweza kutoa nafasi kwa washtakiwa ambao wako tayari kukiri kosa na kushirikiana na vyombo vya dola kwa uwazi ambao ambalo limeelezewa kwamba linachochea utamaduni wa kuwajibika na kuleta ustawi kwa jamii kwa ujumla.

Hata hivyo Anjela Shila aliongeza kwamba mfumo huo wa sheria una manufaa kwa Wakati wa Uchumi Mgumu ambapo kutokana na changamoto za kiuchumi, plea bargaining imekuwa muhimu kwa kuwa inapunguza gharama kwa pande zote.

Alieleza kwamba serikali inapunguza gharama za uendeshaji wa kesi ndefu, na kwa washtakiwa, wanapunguza muda wa kutumia kwenye kesi na kufungua nafasi ya kuendelea na shughuli za kiuchumi.

Kulingana na ujumbe na simu zilizokuwa zikipokelewa katika vituo hoivyo vya Redio vinadhibitisha kwamba Wakazi wa Arusha wameanza kuelewa kuwa mfumo huo unaweza kusaidia kupunguza muda wanaotumia mahakamani, jambo ambalo limepunguza shaka na kuleta matumaini kwa wale waliokuwa wakisubiri mashauri yao kwa muda mrefu.