Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania

Habari

​ELIMU YA AFYA YA AKILI NA MFUKO WA FIDIA KWA WATUMISHI YAWAFIKIA WATUMISHI WA TUMESHERIA.


Mafunzo dhidi ya Afya ya akili na mfuko wa fidia kwawatumishi (WCF) yametolewa kwa watumishi wa Tume ya Kurekebisha Tanzania ili kuwajengea uwezo na kuboresha utendaji kazi wao.

Mafunzo hayo yametolewa leo tarehe 06/12/2023 Katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Tume hiyo ambayo yamehusisha watumishi wote ambapo ilielezwa kwamba Mafunzo hayo yatasaidia watumishi kujua haki zao na namna Serikali inavyoweza kufidia wakipata ulemavu wakiwa Kazini.

Aidha Mafunzo hayo pia yametajwa kusaidia kuboresha afya ya akili navinavyotakiwa kuepukwa Katika kuboresha afya hiyo.

Awali akiwakaribisha watoa mada hao Naibu Katibu Mtendaji Buhran Kishenyi amesema kwamba Tume ya kurekebisha sheria Tanzania imewaalika wataalamu hao ili watumishi watambue haki zao na Kama sehemu ya kutatua changamoto zinazotokana na ajali Kazini pamoja na matatizo yanayosababishwa na Afya ya Akili.

Kwa mujibu wa mtaalamu kutoka Taasisi ya Afya ya akili Milembe Rose Mwangoka amesema Magonjwa ya akili yaliotawala sana kwa sasa ni pamoja na Msongo wa Mawazo, Sonona,Wasiwasi, Matumizi mabovu ya Vilevi pamoja na Skizofrenia ambapo ameeleza husabishwa na matatizo ya kibaolojia, kisaikolojia na kijamii au mazingira.

Akieleza zaidi Rose amesema ili kukabiliana na changamoto hizo namna sahihi ya kujikinga ni pamoja na kupata muda wa kutosha wa kulala, kupenda kushirikisha mtu unaemuamini pindi unapokabiliwa na changamoto pamoja na kupata muda wa kufanya mazoezi ya mwili ili kuimarisha Afya.