Matangazo
UKUSANYAJI MAONI KWA AJILI YA MAANDALIZI YA MPANGO WA MAPITIO YA SHERIA MBALIMBALI
Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania iko katika hatua za awali za Maandalizi ya Mpango wa Mapitio ya Sheria mbalimbali wa mwaka 2023-2025. Lengo la Mpango huu ni kuhakikisha Tanzania inakuwa na Sheria zinazoendana na wakati kwa maendeleo endelevu. Kutokana na Sheria hizi kugusa maeneo mbalimbali, Tume inawaalika wananchi na wadau wote wa sheria kutoa maoni ya sheria na maeneo ya sheria husika yanayoweza kuzingatiwa katika mpango huo.
Ili kuwezesha upatikanaji wa maoni hayo, Tume imeandaa dodoso linalopatikana kwenye Tovuti ya Tume: www.lrct.go.tz. Utabofya sehemu ya Kurasa za Karibu eneo lililoandikwa dodoso la kukusanya maoni ya Mpango wa Mapitio ya Sheria. Dodoso linaweza kujazwa na kuwasilishwa ili kuwezesha kukamilishwa kwa Mpango wa Mapitio ya Sheria. Aidha, maoni yanaweza kuwasilishwa pia kwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania kwa njia ya barua kupitia anuani ifuatayo:
Katibu Mtendaji,
Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania,
Chuo Kikuu cha Dodoma, Jengo la Taaluma, Na. 1,
Shule ya Biashara na Sheria,
S.L.P 1718, DODOMA
Email:lrct@lrct.go.tz