Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania

Habari

WATUMISHI TUMESHERIA WAHIMIZWA KUANDIKA TAARIFA WANAPORUDI KUSHIRIKI MAFUNZO AMA KUSAFIRI NJE YA KITUO CHA KAZI.



Watumishi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania wametakiwa kujenga mazoea ya kuandika taarifa baada ya kukamilisha kazi na baada ya kumaliza Mafunzo kwawanaohudhuriaili kujenga uelewa wa pamoja Katika Taasisi.

Maelekezo hayo yametolewa na Kaimu Katibu Mtendaji Tume hiyo Burhan Kishenyi Leo tarehe 06/12/2023 wakati wa Kikao Cha watumishi wote kilichofanyika Katika ukumbi wa mikutano ofsini hapo ambapo alieleza umuhimu wa kuandika taarifa kwa kila kazi au Mafunzo atakayopata mtu ili kutengeneza kumbukumbu za Taasisi na kuwa na uelewa wa pamoja.

"Wapo watu wanaendaMafunzo ya muda mfupi na mrefu na wengine wakiwa wanasafiri sehemu mbalimbali kwa ajili ya kufanya kazi lakini wakirejea Ofisini hawaandiki taarifa ya walichojifunza(back to office report).

Aidha amehimiza kila mtumishi ambayeatakwenda safari ya kikazi au Mafunzo ndani na nje ya nchi au vikao vya nje ya ofisi wanapaswa kuandika taarifa kueleza yaliojirina kuonesha mapendekezo kulingana na changamoto zilizojitokeza.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mtendaji Zainab Chanzi, amewataka watumishi hao kuongeza juhudi ya kujifunza kutoka kwa wenzao wenye ujuzi ili kuweza kuhamishia ujuzi kutoka mtumishi mmoja hadi mwingine.

Akitolea mfano wa Mafunzo ya mifumo mbalimbali amesema kila mtumishi anatakiwa kujua mifumo unavyofanya kazi hivyo watumishi wanatakiwa kuwa tayari kujifunza kupiatiakwa wenzao hasa Katika kipindi hiki ambapo serikali inafanya kazi kidijitali.

Naye Mwansheria Mwandamizi Dkt kalekwa ameishauri Tume hiyo Kuwekeza kwenye elimuili kupata viwango vya uzamivu ( hard skills )na uwezo au mbinu za kutumia taaluma hizo ( Soft skill).