Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania

Habari

Tume ya Kurekebisha Sheria yawasilisha taarifa ya mapitio ya sheria nane kwa Mh. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Geofrey Pinda


Tume ya kurekebisha sheria imefanikiwa kuwasilisha taarifa ya mapitio ya sheria nane zikiwa ni taarifa ya tathmini ya utekelezaji wa sheria zinazosimamia sekta ya mifugo, tathmini ya utekelezaji wa sheria zinazosimamia adhabu mbadala, tathmini ya utekelezaji wa sheria zinazosimamia sekta ya utalii, taarifa ya mapitio ya mfumo wa sheria zinazosimamia jumuiya tanzania, taarifa za mapitio ya sheria zinazosimamia masoko ya mazao ya kilimo, taarifa ya mapitio ya mfumo wa sheria zinazosimamia wazee wa mahakama, taarifa ya mapitio ya mfumo wa sheria zinazosimamia utatuzi wa migogoro ya kazi na taarifa ya mapitio ya mfumo wa sheria zinazosimamia uwakilishi mahakamani.