Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania

Habari

TUME YA KUREKEBISHA SHERIA TANZANIA YAFANYA KONGAMANO LA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA SHERIA ZA MAKOSA DHIDI YA MAADILI TANZANIA


Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania imefanikiwa kuendesha Kongamano la tathmini ya utekelezaji wa sheria za makosa dhidi ya maadili Tanzania, Kongamano hilo lilifanyika katika Ukumbi wa hoteli ya Morena jijini Dodoma tarehe 05 Aprili 2023, huku mgeni rasmi akiwa ni Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro.

Awali akitoa salamu katika Kongamano hilo, Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bw. Griffin Mwakapeje amesema " lengo la Kongamano hilo ni Tume kupata maoni ya kuwezesha kutimiza majukumu yake ya Kufanya mapitio ya sheria, Kurekebisha sheria, Kufanya maboresho ya sheria katika kulinda na kukuza maadili kwenye jamii ya Taifa letu kwa mujibu wa sheria ya kuanzishwa kwa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania.

Mgeni rasmi wa Kongamano hilo Mhe Waziri Dkt Damas Ndumbaro wakati akifungua Kongamano hilo alisisitiza kufanyika kwa utafiti wa kisheria kabla ya kutungwa kwa sheria ili sheria zitakazotungwa baada ya tafiti zitumike kwa muda mrefu kabla ya kufanyiwa marekebisho.Dkt. Ndumbaro alisema “Kukosekana kwa utafiti wa kisheria hupelekea mabadiliko ya mara kwa mara ya sheria. Hivyo kabla ya sheria kutungwa utangulie utafiti wa kisheria. Sheria zikitungwa baada ya kufanyiwa utafiti hudumu kwa muda mrefu kabla ya kufikiriwa kufanyiwa marekebisho.” katika kutilia mkazo Dr.Ndumbaro alisema Serikali imewasilisha bungeni mapendekezo kuomba Tume ya Kurekebisha Sheria ifanye tafiti kabla ya kutungwa kwa sheria yoyote ili kuepusha marekebisho ya mara kwa mara au kufutwa.

Aidha, Dkt. Ndumbaro ameagiza Tume kuendelea kutoa elimu ya sheria ambapo hadi sasa Tanzania ina jumla sheria 447, “Sheria hizi ni nyingi na wananchi hawatazijua pasipokuwepo na mkakati wa kutoa elimu kwa umma. Na kwa kuzingatia hilo moja ya vipaumbele vya Wizara ya Katiba na Sheria katika Bajeti yake ya mwaka 2023/24 ni kutoa elimu ya sheria na Katiba kwa Watanzania.”

Kongamano hili limekuja wakati muafaka kwani kumekuwepo na ongezeko la vilio kuhusu unyanyasaji mkubwa wa kijinsia na kingono katika jamii. Maoni yatakayotolewa na washiriki katika Kongamano hilo yatasaidia kupaza sauti katika kukabiliana na mmomonyoko wa maadili nchini.

Kwa kuwa Asasi za Kiraia na Wadau wa haki wamekuwa washirika muhimu wakisaidiana na Serikali kukemea ukiukwaji wa haki za binadamu, Dkt. Ndumbaro ametoa wito kwa Wadau kuandaa makongamano kama haya ili elimu na maoni mengi yazidi kutolewa kwa wananchi kuhusu sheria na hivyo kujua haki zao.

" Kwa siku za hivi karibuni watu wameingiza haki za binadamu kwenye masuala ya ushoga na mapenzi ya jinsia moja. Viongozi wa dini na wataalam mtatusaidia kama ni haki za binadamu. Mimi ninavyofahamu hayo ni makosa ya jinai na hayawezi kupata heshima ya kuwa haki za binadamu, Ongezeko la ukiukwaji wa maadili vikiwemo vitendo vya ndoa za jinsia moja na ushoga ni kutokana na utandawazi, lazima tupambane maana utandawazi hauepukiki, kupitia kongamano hili tupate manufaa ya utandawazi ili kudhibiti madhara " alisema. ili kuhakikisha utu wa mtu unaheshimika. sheria mbalimbali zimetungwa kubainisha makosa ya jinai ambayo yanakwenda kinyume na maadili ya jamii". Waziri Ndumbaro alisema Sheria ya Kanuni za Adhabu , Sura ya 16 imeainisha makosa hayo ambayo ni ya kimaadili na hayakubaliki katika jamii, aliendelea kusema tunataka kubadilisha sheria ya kwamba hukumu ile ile ya jinai iweze kuongelea fidia ya muathirika, badala ya muathirika kwenda kufungua kesi nyingine. Hii itasaidia mtu kujua akifanya makosa haya atakwenda jela halafu nyumba yake au kitu chake cha thamani kitauzwa ili kumfidia muathirika, hii itasaidia kuondoa changamoto hizo" alisema Ndumbaro.

Naye Katibu Mtendaji wa Tume ndugu Griffin Mwakapeje alisema maoni yatakayopatikana kupitia kongamano hilo yatawezesha upatikanaji wa tathmini ya sheria zilizopo kama zina changamoto zifanyiwe marekebisho ili ziwe bora na kulinda utamaduni, mila na desturi za Watanzania.

Jaji Mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Januari Msoffe alishauri sheria zilizopo ziendane na wakati na zifanyiwe tathmini