Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania

Habari

​TUDUMISHE USHIRIKIANO ILI KUONGEZA UFANISI- MANDEPO



Katibu Mtendaji Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT) Bw. George Mandepo ameiomba Tume ya Kurekebisha Sheria ya Zanzibar kuendeleza ushirikiano wa Tume hizo hasa katika kujengeana uwezo katika maeneo mbalimbali ya utekelezaji wa majukumu yao ili kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa majukumu ya Tume hizo.

Rai hiyo ameitoa leo tarehe 05/02/2024 wakati wa kikao kifupi kilichofanyika ofsini kwake mara baada ya kutembelewa na Timu kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar ikiongozwa na Mkurugenzi wa Mapitio na Marekebisho ya Sheria Dkt. Mahfoudha Masoud Ally ambapo waliweza kubadilishana nyaraka mbalimbali zikiwemo taarifa za utafiti na majarida.

Bw. Mandepo ameeleza kwamba “tuendelee kushirikiana hasa katika eneo la kujengeana uwezo ili tuweze kufanya kwa ufanisi mkubwa kile ambacho kinatarajiwa ikiwa ni pamoja na kubuni mbinu za kuwa “Proactive” badala ya “reactive” alisema Mandepo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mapitio na Marekebisho ya Sheria wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar, Dkt. Mahfoudha Masoud Ally baada ya kubadilishana nyaraka alisema, Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar inatambua umuhimu wa ushirikiano na Tume ya Kurekebisha Sheria hivyo basi nyaraka na machapisho waliyoyapokea yatakuwa nyenzo muhimu katika utekelezaji wa majukumu ya Tume na hivyo kusaidia kupata matokeo mazuri katika mchakato wa marekebisho ya sheria.

MWISHO