Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania

Habari

​LRCT yashiriki maadhimisho ya wiki ya sheria 2025



Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT) imeshiriki Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yaliyofanyika kitaifa mkoani Dodoma kwa lengo la kuelimisha umma kuhusu shughuli zake, kutoa ushauri wa kisheria, na kukusanya maoni kuhusu mabadiliko ya sheria mbalimbali nchini.

Katika maadhimisho hayo, ambayo kawaida huandaliwa na Mahakama ya Tanzania, Tume ilipata fursa ya kuelezea tafiti zilikwishafyika na umuhimu wake kwa jamii ikiwa ni pamoja na kupokea mrejesho kutoka kwa wananchi, wadau wa sheria, na taasisi mbalimbali.

Aidha viongozi mbalimbali walitembelea banda la Tume hiyo na kushauri maboresho kadhaa katika upokeaji wa maoni na utoaji wa mresjesho kwa wananchi baada ya maboresho ya sheria hizo.

Hata hivyo banda la Tume lilihudumiwa na wataalamu wa sheria waliotoa msaada wa kisheria kwa wananchi waliotembelea. Pia, Tume ilitumia fursa hiyo kusambaza nyaraka na machapisho mbalimbali yanayohusu marekebisho ya sheria ili kuongeza uelewa wa umma.

Maadhimisho ya Wiki ya Sheria ni sehemu muhimu ya jitihada za kuimarisha utawala wa sheria nchini Tanzania, na ushiriki wa Tume ya Kurekebisha Sheria unaonyesha dhamira yake ya kuhakikisha sheria zinaendana na mahitaji ya jamii.