Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania

Miradi Inayoendelea

Mapitio ya Mfumo wa Sheria Zinazosimamia Uwakilishi Mahakamani Tanzania


Mapitio ya Mfumo Sheria Zinazosimamia Uwakilishi Mahakamani Tanzania

Mapitio ya Mfumo wa Sheria Zinazosimamia Uwakilishi Mahakamani Tanzania ni mradi unaofanywa na Tume. Huu ni miongoni mwa miradi iliyoainishwa kwa ajili ya mapitio hadi kufikia 2023 katika Mpango Mkakati wa Muda wa Kati wa Tume wa Miaka mitano ulionza kutekelezwa mwaka wa fedhawa 2018/19 hadi 2022/23.

Mpango Mkakati unalengo la kufikia lengo kuu la Tume ambalo ni kuboresha utawala wa sheria unaoweka mazingira wezeshi yenye kuipeleka Tanzania katika viwanda vya kati kufikia 2025 kulingana na Mpango wa Maendeleo wa 2025.

Lengo la utafiti huu ni kupitia Mfumo wa Sheria Unaosimamia Haki ya Uwakilishi kwa lengo la kuainisha changamoto zinazokwamisha upatikanaji wa haki ya uwalikishi. Utafiti huu pia utawezesha kufanyika kwa maboresho muhimu katika kuimarisha upatikanaji wa haki ya uwakilishi katika mfumo wa utatuzi wa migogoro.