Tume Yashiriki Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania inashiriki katika maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyoanzaa tarehe 16-23 Juni 2014, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar Es Salaam.

Katika Maonesho hayo Tume inatoa huduma mbalimbali kwa wananchi ambazo ni pamoja na:

  • Kutoa elimu na ushauri wa kisheria kwa wananchi;
  • Kuonyesha kazi mbalimbali ambazo Tume imezifanya na kazi ambazo zinaendelea;
  • Kupokea maoni kutoka kwa Wananchi kuhusiana na sheria mbalimbali zinazohitaji maboresho.

Kauli mbiu ya Wiki ya Utumishi wa Umma ni 『Mkataba wa Misingi na Kanuni za Utumishi wa Umma Barani Afrika ni Chachu ya Kuimarisha Utawala Bora na Uendeshaji wa Shughuli za SerikaliĀ  kwa Uwazi』.

Maadhimisho ya ya Wiki ya Utumishi wa Umma huadhimishwa na nchi zoteĀ  Barani Afrika ambapo hutumika pia kuzipatia tuzo taasisi za umma zinazoonesha ubunifu katika kutoa huduma kwa wateja na wananchi kwa ujumla.

Aidha, katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma kutakuwa na Kongamano la Miaka 50 la Muungano katika Utumishi wa Umma litakalofanyika katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere Dar es Salaam kuanzia tarehe 19-20 Juni 2014 ambapo kongamano hilo litafunguliwa na Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe Celina Kombani na kusimamiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Ombeni Sefue.

 

Ni matumaini ya Tume ya kurekebisha Sheria Tanzania kuwa maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yatakuwa njia mojawapo ya kuiwezesha Tume kujitangaza pamoja na kupata maoni mbalimbali kuhusiana na sekta ya sheria na baadaye Tume kuyafanyia kazi na kuwa na sheria zitakazoendana na wakati.

 

Powered by WordPress | Designed by: Premium WordPress Themes | Thanks to Themes Gallery, Bromoney and Wordpress Themes