JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA KUREKEBISHA SHERIA.

 

UTAFITI WA SHERIA ZINAZOSIMAMIA HUDUMA ZA WAZEE MIKOA YA PWANI, LINDI NA MTWARA

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania ni Idara ya Serikali inayojitegemea chini ya Wizara ya Katiba na Sheria iliyoanzishwa na Sheria ya Tume ya Kurekebisha Sheria Namba 11 ya mwaka 1980. Kwa mujibu wakifungu cha 4 cha Sheria inayoanzisha Tume, moja ya jukumu kubwa la Tume hii nikufanyia Mapitio na Utafiti Sheria au eneo lolote la Sheria nchini na kuwasilisha mapendekezo Serikalini yanayolenga kuboresha sheria hizo.

Kwa kuzingatia hilo, Tume inatekeleza mapitio ya Sheria mbalimbali moja wapo ikiwa ni Mapitio ya Mfumo wa Sheria zinazohusu utoaji huduma kwa Wazee (Social Adult Care) nchini. kwa sasa Tume inaendelea na ukusanyaji wa maoni ya Wadau mbalimbali Mikoani ikiwa ni awamu ya tatu baada ya kukamilisha kanda ya Kaskazini na Kanda ya Ziwa. Katika hatua hii, Tume  itafanya ziara ya kukusanya maoni katika Mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara. Katika ziara hiyo, Tume inatarajia kukutana na Wadau mbalimbaliili kupata maoni yao juu ya namna ya kuboresha Sheria husika. Ratiba ya ziara ni kama ifuatavyo;

18/08/2014   –         Kibaha

19/08/2014   –         Kisarawe

21/08/2014   –         Lindi

22/08/2014   –         Mtwara

26/08/2014   –         Nachingwea

29/08/2014   –         Masasi

Tume inatarajia ushirikiano kutoka kwa Wadau mbalimbali katika mikoa na wilaya husika wakati wa ziara ya Tume. Pia kwa wale ambao hawatapata nafasi ya kuonana na ujumbe wa Tume, tafadhali wasilisha maoni yako kwa anuani zifuatazo:

Anuani ya posta:     Katibu Mtendaji, Tume ya Kurekebisha Sheria

P.O.Box 3580, Dar es Salaam.

Simu: 0222123533:       Nukshi (Fax):    022212354

Barua pepe:  maoni@lrct.go.tz au lrct@lrct.go.tz

Powered by WordPress | Designed by: Premium WordPress Themes | Thanks to Themes Gallery, Bromoney and Wordpress Themes