TAARIFA KWA UMMA

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (Tume) ilianzishwa mwaka 1983 na Sheria ya Tume, Sura 171 [Mapitio ya 2002].  Tume hii ni taasisi ya Serikali inayojitegemea iliyo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria.Jukumu kuu la Tume ni kupitia na kufanyia utafiti sheria zote za nchi kwa dhumuni la kuziboresha iliziendane na wakati. Katika kupitia sheria zote za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tume hufanya utafiti kwenye maeneo mbalimbali ya sheria kwa nia ya kubainisha mapungufu yaliyopo na hatimaye kutayarisha taarifa yake yenye mapendekezo ya namna ya kuboresha sheria husika.Kwa mujibu wa kifungu cha 14 cha Sheria ya Tume ya Kurekebisha Sheria,  Tume inatakiwa kuwasilisha taarifa yake ya utafiti yenye mapendekezo kwa Waziri anayehusika na mambo ya sheria.

 

Tume inatekeleza Miradi mbalimbaii ya mapitio ya Sheria mbalimbali.Hata hivyo  sasa Tume imekamilisha miradi yake miwili ya Mapitio ya Mfumo wa Sheria unaosimamia Haki za Madai (Civil Jusice System) pamoja na Mapitio yaSheria zinazosimamia Mfumo wa Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi( Legal Framework on Land Dispute Settlement.Mapitio haya ya Sheria na Mifumo  yanalenga maboresho ya Sheria Mbalimbali.

 

 1. 1.   MAPITIO YA MFUMO WA SHERIA UNAOSIMAMIA HAKI ZA MADAI (CIVIL JUSICE SYSTEM)

Katika kufanya mapitio na utafiti wa Sheria  Tume iliwahusisha wadau mbalimbali wakiwemo Mahakama na Mabaraza, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu,Taasisi zisizo za serikali, Jumuiya za Wafanyabiashara, Madalali,  Mawakili na Taasisi na Idara za Serikali.

 

Katika kufanya utafiti, Tume ilijikita katika kuboresha na kufikiamisingi ya utoaji  yaani 「haki sawa kwa wote na kwa wakati」 kama ilivyobainishwa na Ibara 107A ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.  Misingi hii ni:-

 • usawa – kutenda haki kwa wote bila kujali hali ya mtu kijamii au kiuchumi.
 • uharaka – kutochelewesha haki bila sababu ya msingi.
 • haki –  kutoa fidia ipasayo kwa wakati na thamani halisi kwa watu wanaoathirika kutokana na makosa ya watu wengine, na kwa mujibu wa sheria mahususi iliyotungwa na Bunge.
 • usuluhishi –  kukuza na kuendeleza usuluhishi wa haraka na rahsi baina ya wanaohusika katika migogoro; na

 

Mradi huu ulihusisha Mapitio ya Sheria tisa (9) na kanuni nane (8) zifuatazo:-

 

1.Sheria ya Mamlaka ya Rufani, 1979 [Sura 141 Mapitio ya 2002]

 1. Sheria ya Usuluhishi, 1931 [Sura 15 Mapitio ya 2002]
 2. Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Madai, 1966 [Sura 33 Mapitio ya 2002]
 3. Sheria ya Ushahidi, 1967 [Sura 6 Mapitio ya 2002]
 4. Sheria ya Mashauri Dhidi ya Serikali, 1967 [Sura 16 Mapitio ya 2002]
 5. Sheria ya Mahakama za Ardhi, 2002
 6. Sheria ya Ukomo wa Mashauri, 1971 [Sura 89  Mapitio ya 2002]
 7. Sheria ya Mahakama za Mahakimu, 1984 [Sura 11 Mapitio ya  2002]
 8. Sheria ya Mabaraza ya Kata, 1985 [Sura 206 Mapitio ya 2002]

 

Kanuni

 1. Mwenendo wa Mashauri ya Madai kwenye Rufaa zinazo tokea Mahakama ya Mwanzo) Kanuni (Tangazo Na. 312 la Mwaka 1964)
 2. Tozo za Ada kwenye Mahakama Kuu (Kitengo cha Biashara), 1999 (Tangazo Na. 275 lillilofanyiwa marekebisho na Tangazo Na. 428 la mwaka 2005)
 3. Madalali wa Mahakama Juu ya Uteuzi Wao, Malipo, na Udhibiti wa Nidhamu (Tangazo Na. 315 la Mwaka 1997);
 4. Likizo za Mahakama (Tangazo Na. 307 la Mwaka1964)

 

Tume imefanya utafiti kwenye sheria zinazosimamia Haki za Madai kwa kubainisha mapungufu yaliyopo na kutoa mapendekezo ya namna bora ya kuboresha mapungufu husika.

 

1.1 Mapungufu katika Mfumo wa Kesi za Madai

Baadhi ya Mapungufu yaliyobainishwa :

 • Ucheleweshwaji wa usikilizaji wa Kesi na utoaji wa Hukumu
 • Uhaba wa Mahakimu na Majaji
 • Uhaba wa vitendeakazi na fedha kwa upande wa Mahakama
 • Uahirishwaji wa kila mara wa  Kesi
 • Mapungufu katika Nyaraka zinazowasilishwa Mahakamani (Pleadings)
 • Mapungufu ya Sheria na Utekelezaji
 • Ukiukwaji maadili ya kitaaluma ikiwemo Rushwa katika Sekta ya Sheria

 

1.2 Mapendekezo ya Tume :

Tume imependekeza marekebisho na Maboresho ya Sheria mbalimbali ili kurahisisha upatikanaji wa haki katika kesi za madai kwa haraka na rahisi ili wananchi waendelee na shughuli za uchumi badala ya kupoteza muda mwingi mahakamani.Moja ya Mapendekezo hayo ni :

 • Kupunguza uahirishwaji wa Kesi
 • Kuruhusu Mawakili kwenda hadi Mahakama za Mwanzo sambamba na kuajiri Mahakimu wenye Shahda ya Sheria Mahakama za Mwanzo
 • Kuruhusu na kukubali Ushahidi wa Teknoljia katika maeneo yote ya Sheria
 • Kuruhusu uwasilishwaji wa Nyaraka za Mahakama kupiti mtandao
 • Kuboresha Mfumo wa Mashauri nje ya Mahakama (ADR)
 • Kitengo cha Mahakama Kuu kianzishwe katika kila Mkoa sambamba na Mjaji wa utosha
 • Kuongeza idadi ya Mahakimu, Majaji na Mawakili
 • Mafunzo yatolewe kwa Mahakimu, Majaji, Wasajili na Mawakili
 • Kuwe na ukomo maalumu wa mwisho wa kusikilza kesi pamoja na ukomo wa Rufaa katika Mahakam azote isipokuwa tu kama kuna ulazima wa kuongeza muda
 • Kusikiliza Kesi kwa kuzingatia matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Mungano
 • Sheria zinazosimamia Madalali ziboreshwe

Tume imewasilisha taarifa ya Utafiti kwa Waziri wa Katiba na Mambo ya Sheria kwa hatua zaidi chini ya kifungu cha 15 cha Sheria ya Tume ya Kurekebisha Sheria.

 

2.0 MAPITIO YA MFUMO WA UTATUZI WA MIGOGORO YA ARDHI

 

2.1 Matokeo ya Taarifa ya  Mapitio Ya Mfumo Wa Utatuzi Wa Migogoro Ya Ardhi

Tanzania ina sheria mbalimbali zinazosimamia masuala ya ardhi zikiwemo zile zinazoratibu Taasisi za usuluhishina  utatuzi wa Migogoro ya Ardhi.

 

Kimsingi mahakama zote zimekuwa na Mamlaka ya kusikiliza mashauri yanayohusiana na    migogoro ya Ardhi hadimiaka ya tisini ambapo ambapo Sera ya Ardhi ilipotungwa na hivyo kupelekea mabadiliko ya Sheria za Ardhi na Sheria zinginezo..Hata hivyo kutokana na matatizo ya uhaba wa fedha na raslimali watu, Mahakama zetu hazikupata fursa ya kuendelezwa na kuimarishwa kwa kasi inayolingana na ongezeko la mahitaji halisi ya kijamii katika masuala ya ardhi.

Kwa kuzingatia hilo sheria kuu mbili za Ardhi (Sheria ya ArdhiNa.4  na Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na.5) zilitungwa mwaka 1999.Sambamb na Sheria hizi, pia sheria inayohusu mfumo wa utatuzi wa migogoro ya Ardhi (The Courts, Land Dispute Settlement Act) ilitungwa mwaka 2002.Mabadiliko haya yote ya Sheria yalipelekea kuanzishwa Mabaraza ya Ardhi toka ngazi ya Vijiji hadi Mkoa.Sheria hii inayapa  Mabaraza haya mamlaka ya kusikiliza mashauri yoteyanayohusiana  na  ardhi kwa lengo la kupunguza mlundikano wa kesi na migogoro ya Ardhi.Pia katika ngazi ya Mahakama Kuu kilianzishwa Kitengo maalum kusilikiza mashauri ya ardhi pamoja na  kusikiliza rufaa zote za kesi za ardhi zilizotoka katika Mabaraza ya Ardhi (Land Tribunals).

2.2       Kuendelea kwa Migogoro ya Ardhi na Tume imefanya nini

Pamoja na mabadiliko hayo ya sheria yaliyofanyika katika  mfumo mzima wa utatuzi wa migogoro ya ardhi, bado migogoro ya ardhi inaendelea na hata kupelekea  wananchi wengi kupoteza maisha na mali zao ikiwemo ardhi.Pia Mabaraza haya yamekuwa na changamoto nyingi ikiwemo kukosekana kwa usimamzi wa Mabaraza haya toka kwa Mahakama za Juu. Tume ya Kurekebisha Sheria kwa kutumia mamlaka yake ya kisheria, ilifanyia mapitio Sheria na Mfumo mzima wa utatuzi wa Migogoro wa migogoro ya Ardhi.Katika kufanikisha mapitio ya sheria na utafiti, Tume iliwahusisha wadau mbalimbali katika mikoa mbalimbali ya Tanzania kwa lengo la kupata maoni zaidi yatakayopelekea mabadiliko ya Sheria na Mfumo wa utatuzi wa Migogoro ya Ardhi. Katika utafiti wake Tume iliwahusisha wadau mbalimbali wakiwemo wanasheria, Mahakama, Wizara ya Ardhi, Taasisi zisizokuwa za kiserikali (NGOs) pamoja na mabaraza ya ardhi ya vijiji, kata na mkoa.

Utafiti katika eneo hili pia ulilenga katika kufanya tathmini  ya utekelezaji wa sheria hizi na kubaini mapungufu yanayojitokeza wakati wa kutekeleza sheria hizo na kutoa mapendekezo kwa serikali kwa lengo la kuondoa dosari za kisheria na kiutekelezaji zilizojitokeza, ili malengo na makusudio ya sheria hiyo yaweze kutekelezwa kwa ufanisi  na mafanikio zaidi kama ilivyokusudiwa

 

Kwa kurekebisha na kuboresha mfumo wa sheria zinazosimamia utatuzi wa migogoro ya ardhi serikali itakuwa imefikia malengo yafuatayo:

 • Utatuzi na usuluhishi wa migogoro ya Ardhi mapema iwezekanavyo ambapo kutachangia ukuaji wa Uchumi.
 • Utatuzi na usuluhishi wa migogoro ya Ardhi mapema iwezekanavyo kutadumisha ushirikiano na amani kati ya wakulima na wafugaji na serikali kwa ujumla.
 • Maamuzi ya haraka na kwa wakati yataondoa tatizo la urasimu uliopo, vikwazo na mlundikano wa kesi.
 • Itapunguza gharama za kiutawala kwa kuwa na Wizara moja itakayosimamia utatuzi wa migogoro ya ardhi.

 

2.3       Changamoto na matatizo yaliyobainishwa

Tume ilibaini mapungufu mbalimbali ya kisheria, kisera nakiutekelezaji.Mapungufu haya yamepelekea migogoro ya ardhi kuendelea kuongezeka na kupelekea wananchi kuanza kukosa imani na mfumo wa utatuzi wa Migogoro ya Ardhi uliopo.Matumizi ya ardhi pia yameongezeka sambamba na ongezeko la watu, hifadhi za misitu, hifadhi za Taifa, na wakati mwingine katika hali inayoleta migogoro ya matumizi ya ardhi baina ya watumiaji.

Kwa upande mwingine mabaraza hayo machache ya Wilaya/Mkoa yalilemewa na wingi wa rufaa kutoka Mabaraza ya Kata.

Pia utafiti ulionyesha kuwa  majaji wachache wa kitengo cha  Ardhi, walishindwa kuhimili wingi wa rufaa zilizotoka kwenye mabaraza (mangapi) machache yaliyokwishaanzishwa.Hata hivyo kuna mabadiliko yaliyofanyika Mahakamani ambapo sasa Majaji wote wana uwezo wa kusikiliza mashauri yanayohusu  migogoro ya  ardhi.

Wananchi walipendekeza pamoja na mambo mengine sheria zilizopo zifanyiwe marekebisho sambamba na kuboresha mfumo mzima wa Utatuzi wa Migogoro.Pia ilipendekezwa kuwa Serikali iangalie uwezekano kuunganisha mabaraza haya na ahakama za kawaida ili kuwa na usimamizi mzuri toka ngazi ya chini hadi ngazi za juu za Rufaa.Yapo matatizo yanayohitaji mabadiliko ya sheria kwa mfano kuruhusu Mahakama za kawaida kuendelea kupokea na kusikiliza mashauri pale ambapo mabaraza hayajaanzishwa, lakini pia yapo yanayohitaji kufikiriwa upya kisera, pengine kurejesha mfumo mmoja wa utatatuzi wa migogoro chini ya mahakama.Mapendekezo yetu yanatokana nakutambuzi wa uwepo mabadiliko makubwa katika Nyanja ya kiuchumi, kisera na kijamii. Tume ilikamilisha Taarifa ya Utafiti yenye mapendekezo na kuiwasilisha kwa Waziri wa Katiba na Sheria mwezi Meimwaka huu 2014.

 

Imetolewa na:

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania

09 Septemba, 2014

 

Powered by WordPress | Designed by: Premium WordPress Themes | Thanks to Themes Gallery, Bromoney and Wordpress Themes