TUMESHERIA SPORTS CLUB YASHIRIKI MASHINDANO YA SHIMIWI MKOANI MOROGORO

Timu ya TUMESHERIA Sports Club yashiriki michezo ya SHIMIWI iliyoanza rasmi tarehe 27 Sept 2014 katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.

Michezo hiyo inayowakutanisha Watumishi wa Serikali kutoka katika Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala wa Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa itahitimishwa Oktoba 11, 2014.

Jumla ya Watumishi 3,500 kutoka katika vilabu 71 vilivyothibitisha kushiriki ambavyo ni Wizara 26, Mikoa 25, Idara zinazojitegemea 12 na Wakala wa Serikali 8 wanategemea kushiriki katika michezo ya mpira wa miguu, Netboli, kuvuta kamba, Riadha, Karata, Bao, Draft, Baiskeli na Darts.

Powered by WordPress | Designed by: Premium WordPress Themes | Thanks to Themes Gallery, Bromoney and Wordpress Themes